TRA

TRA

Friday, August 4, 2017

MSUVA AZIDI KUNG’ARA MOROCCO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


msuva difaa al jadidi #salehjembe
Mshambulizi Saimon Happygod Msuva ameendelea kung’ara kisoka baada ya kufunga mabao mawili katika mechi yake ya tatu ya kirafiki waliyocheza jana.
Mechi hiyo ni ya kirafiki mazoezi na ilichezwa jana na Difaa Al Jadid ya Morocco anayoichezea ilishinda kwa mabao 3-0.
Kabla ya mechi hiyo, juzi walicheza mechi mazoezi nyingine na kutoka sare ya bao 1-1, Msuva akiwa amesababisha penalti iliyozaa bao la Difaa Al Jadid.
Mechi ya kwanza ya kirafiki aliyocheza dakika 45, Msuva alifunga bao la kufutia machozi wakati Difaa Al Jadid ikilala kwa mabao 2-1.
Msuva amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga ambayo aliisaidia kubeba makombe mfululizo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger