Mhandisi Baraka Felix kutoka
Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea
eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani
Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha
sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Mhandisi Baraka Felix kutoka
Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea
kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa
maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na
Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na
Serikali .
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kutembelea
eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani
Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha
sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (kushoto) akipokea maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega,
Anderson Njiginya wakati alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji
cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na
Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na
Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto)
akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Busega mara baada ya
kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi,
Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli
kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, (kushoto) Mkuu wa
Wilaya hiyo, Mhe.Tano Mwera.
Msajili Msaidizi wa Baraza la
Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja
mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao
cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina
Mabula(Mb) na watumishi hao Wilayani Busega(hawapo pichani).
………………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri
nchini, kuyatambua na kuyatolea taarifa maeneo yanayohodhiwa na watu
bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara iweze
kuchukua hatua stahiki.
Naibu Waziri huyo ameyasema
hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya
Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati
Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha
Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji
katika eneo hilo utakaonufaisha vijiji vinne vya kata ya Lamadi.
Mhe.Mabula amesema Halmashauri
zinapaswa kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha
sheria na kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo
ya Makazi ili yaweze kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi
mengine yenye manufaa zaidi kwa jamii.
“Maeneo yote yaliyohodhiwa
ambayo hayajaendelezwa na ambayo pengine hayakupatikana kihalali, ni
jukumu la Halmashauri kuyatambua na kuleta taarifa zake Wizarani ili
Wizara iweze kuchukua hatua ya kuweza kuyarudisha katika matumizi kwa
Umma na yaweze kufaidisha watu wengi zaidi badala ya mtu mmoja” amesema
Naibu Waziri Angelina Mabula
Aidha,Naibu Waziri Mabula
amebainisha sababu zilizopelekea Mwekezaji Hermati Pateli kufutiwa hati
ya eneo hilo na Serikali kuwa ni udanganyifu wa Uraia pamoja na
upatikanaji wa hati ambao haukuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Naibu Waziri huyo amesema eneo
lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji huyo isivyo halali ambalo
limefutiwa hati miliki limegawanyika katika ploti mbili, ploti Namba 01
na Namba 02 Block C lenye ukubwa wa hekta 7.62 na Block Namba 03 C
hekta 5.45.
Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb),
Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji wa Lamadi kutoka Kampuni ya EAU
Consult, Baraka Felix amesema Tanki la Maji litakalojengwa katika eneo
hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 3000 kwa siku.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya amesema Mradi wa
Maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo hilo utawanufaisha wananchi wa
Vijiji Vinne vya Kalago, Lamadi, Lukungu na Mwabayanda.
Mradi huu wa maji unaojengwa
katika eneo hili lililokuwa linamilikiwa isivyo halali na Mwekezaji
Pateli, utagharimu kiasi cha Yuro milioni 2.8, na unatarajiwa kukamilika
ifikapo Mei, 2019.
SHARE








No comments:
Post a Comment