Cristiano Ronaldo
alifunga bao lakini baadaye akafukuzwa uwanjani huku Real Madrid
wakilaza Barcelona 3-1 katika Super Cup ya Uhispania, mechi ya mkondo wa
kwanza.
Ronaldo, aliyeingia kama nguvu mpya alirejesha Real Madrid mbele alipokimbia kutoka katikati ya uwanja na kufunga.
Alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati lake kusherehekea.
Muda mfupi baadaye, alioneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kujiangusha na akafukuzwa uwanjani.
Marco Asensio alifunga la tatu.
- Barcelona wamchukua tena Deulofeu
- Neymar: Nahitaji changamoto mpya
- PSG wamnunua Neymar kwa rekodi ya dunia ya £200m
Ronaldo alikaa dakika 24 pekee uwanjani.
Barcelona walionekana kutatizika bila Neymar ambaye alihamia Paris Saint Germain kwa rekodi ya dunia ya £200m.
Real watakuwa wenyeji wa Barca mechi ya marudiano Jumatano saa 22:00 BST (saa sita usiku saa za Afrika Mashariki). Barcelona walimchezesha Gerard Deulofeu safu ya mashambulizi pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment