JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo : “N G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463 Sanduku la Posta 9203,
Telex : 41051 DAR ES SALAAM, 25 Agosti, 2017.
Tele Fax : 2153426
Barua pepe : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananch wa
Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya siku ya majeshi
yanayoanza tarehe 25 Agosti 2017. Sherehe hizi ni za
kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) ambazo hufanyika kila mwaka tarehe 01Septemba, mwaka huu
sherehe hizo zitaadhimishwa wakati Jeshi linatimiza miaka 53 tangu
lilipo asisiwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza Marehemu Baba wa
Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere Septemba Mosi 1964.
Mwaka huu 2017 maadhimisho hayo
yatafanyika kwa wanajeshi kufanya shughuli mbalimbali kuanzia tarehe 25
Agosti 2017 hadi tarehe 31 Agosti 2017 na kilele cha maadhimisho hayo
kitakuwa tarehe 01 Septemba 2017.Shughuli hizo ni pamoja na kufanya
shughuli za huduma za kijamii katika maeneo jirani na vikosi vya Jeshi,
Wanajeshi kuchangia damu salama katika hospitali mbalimbali nchini,
kutoa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa Dar es salaam huduma za tiba
zitatolewa katika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 2:00 asubuhi siku
ya tarehe 01 Septemba, aidha wanajeshi watafanya michezo mbalimbali na
wananchi Pamoja na kushiriki kufanya usafi kwenye maeneo ya kijamii
(Hospitali, Masoko, Mashule n.k) na pia watafanya michezo Shirikishi na
jamii inayowazunguka.
Kauli Mbiu ya maadhimisho haya ni Wiki ya Majeshi na Afya yako.
Imetolewa na Kurugenzi
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
SHARE









No comments:
Post a Comment