Moja kati ya stori ambazo zimewashitua wengi Ijumaa ya leo
September 1 2017 ni kuhusiana na maamuzi ya Mahakama Kuu nchini Kenya
kubatilisha matokeo ya uchaguzi Mkuu uliyofanyika August 8 2017 na Uhuru
Kenyata kuibuka mshindi wa Urais dhidi ya Raila Odinga.
Jaji Mkuu David Maraga ameagiza uchaguzi Mkuu mpya utafanyika
ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria na katiba na umebatilishwa kwa
sababu IEBC hawakuwa wameandaa uchaguzi huru na haki. Kila mmoja
amepokea uamuzi huo kitofauti, mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ameandika mtazamo wake kupitia ukurasa
wake wa instagram “Niliwahi Sema najifunza jambo toka Kenya, Leo
inathibitika wakati Mahakama inafungua kurasa Mpya ya Kumbukumbu ya
Maamuzi.#KenyaDecides“
No comments:
Post a Comment