Mechi ya Arsenal dhidi ya Cologne katiika kombe la Yuropa ilikumbwa na ghasia na kusababisha kucheleweshwa kwa saa moja.
Maafisa wa polisi walisema kuwa watu watano walikamatwa kwa tuhuma kuhusika katika ghasia.
Kulikuwa hakuna ripoti zozote za ghasia wakati wa mechi hiyo ambayo Arsenal ilishinda 3-1.
Timu hiyo ya Ujerumani ilikuwa imepewa tiketi 2,900 pekee.
Lakini takriban mashabiki 20,000 wa timu hiyo waliingia na kusimamisha biashara mjini London nyakati za mchana Alhamisi.
Hatahivyo hivyo mechi hiyo ilianza baada ya kucheleweshwa kwa saa moja.
CHANZO:BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment