Ripoti za hivi
punde kutoka nchini Uingereza zinasema kuwa mlipuko umetokea kwenye
treni zinazokwenda chini kwa chini katika eneo la Kusini magharibi mwa
mji mkuu wa London.
Idara za kutoa huduma ya dharura zimewasili katika eneo hilo.
Picha zimeonyesha ndoo nyeupe ikichomeka ndani ya mfuko wa duka la jumla ,lakini mfuko huo hauonyeshi uharibifu mkubwa ndani ya treni hiyo.
Mashahidi wameelezea kuona abiria mmoja akiwa na majeraha ya uso.
Mafisa wa zima moto wakiwasili katika eneo la mlipuko nchini Uingereza
Wengine wamesema kuwa kulikuwa na wasiwasi huku abiria wakitoka ndani ya treni hiyo katika kituo cha treni cha Parsons Green.
Huduma ya ambalensi inasema kuwa imetuma kikosi cha kukabiliana na majanga katika eneo hilo.
Mtangazaji wa BBC Riz Lateef aliyekuwa katika kituo hicho cha treni akielekea kazini alisema: kulikuwa na wasiwasi mwingi huku watu wakitoka ndani ya treni hiyo wakihofia maisha yao huku wakisema kulikuwa na mlipuko.
Wengi walipata majeraha ya kukatwa wakijaribu kutoroka eneo hilo. Mwandishi wa BBC Sophie Raworth anasema kuwa alimuona mwanamke mmoja akiwa na majareha ya moto usoni na miguuni.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment