Mkuu wa mkoa wa Pwani
,mhandisi Evarist Ndikilo ,akionyesha eneo la mradi litakapozalisha
umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao
utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme.(Picha na Mwamvua
Mwinyi )
Eneo la mradi litakapozalisha
umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Dam),ambao
utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawatts 2,100 za umeme,linavyoonekana
.(Picha na Mwamvua Mwinyi )
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi
Evarist Ndikilo ,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho
karibu na pori la akiba la Selou .(Picha na Mwamvua Mwinyi )
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,na ujumbe wake wakikagua eneo la mto huo.(Picha na Mwamvua Mwinyi )
………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi ,Rufiji
Wakazi wa wilaya ya
Rufiji ,Mkoani Pwani pamoja na watanzania kijumla wanatarajia kunufaika
na mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji
(stiegler’s gorge hydropower dam project),ambao utakuwa na uwezo wa
kuzalisha megawatts 2,100 .
Mradi huo utazalishwa kutoka chanzo hicho , katika pori la akiba la Selou Kanda ya Kaskazini (Matambwe ).
Kwasasa nchi inazalisha
megawatts 1,450 lakini Stiegler’s gorge itazalisha megawatts 2,100
hali itakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi .
Akizungumza mara baada
ya kwenda kukagua na kujiridhisha eneo utakapozalishwa mradi huo kabla
ya utekelezaji kuanza,Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo,
alisema tangazo rasmi limeshatolewa na wizara ya nishati na madini tangu
august 30 mwaka huu.
Aidha alifafanua ,tangazo hilo linawapa nafasi kwa makampuni ya ujenzi wa mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme .
Mhandisi Ndikilo,alibainisha kampuni yoyote iwe ya ndani ama nje ya nchi ikikidhidhi vigezo itatangazwa .
Alieleza endapo mradi utakamilika utawezesha kuwepo kwa umeme wa uhakika na kuvutia wawekezaji kwa wingi.
Mhandisi Ndikilo
,alisema wilaya ya Kisarawe na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kibiti na
Rufiji umeme ukatikakatika hivyo kuna changamoto ya upungufu wa umeme
hali inayokwamisha jitihada za kuinua sekta ya uwekezaji na viwanda .
“Tatizo la umeme bado
ni kubwa mkoani hapa licha ya mkoa huu kusheheni viwanda “Mradi umekuja
muda muafaka ambapo mkoa huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda ”
alifafanua .
Faida moja wapo ya
mradi ni kuwa na maji mengi ya kunywa na viwandani kwa mikoa ya Pwani
,Dar es salaam na Morogoro ,utaliii ,maji kwa ajili ya wanyama pori na
kilimo .
Mhandisi Ndikilo
alieleza ,mradi umekuja muda muafaka na umefika mahala pake ,ambapo Mkoa
huo umejipanga kuwa ukanda wa viwanda .
“Ni nia ya serikali ya
awamu ya tano kuhakikisha mawazo ya baba wa taifa hayati mwl .Julius
Nyerere ya tangu mwaka 1980 juu ya kuzalisha umeme kutoka katika
maporomoko ya mto huo yanatekelezwa kwa haraka iwezekanavyo “alisema
mhandisi Ndikilo .
Baada ya kutembelea
eneo la mradi mhandisi Ndikilo ,alipata fursa ya kwenda kuzungumza na
wakazi wa kijiji cha Mloka kilicho mpakani na pori la akiba la Selou .
Mhandisi Ndikilo, alisema ujenzi wa mradi huo utafungua milango ya kiuchumi na ujasiriamali na kibiashara .
Kwa upande wa wakazi wa Mloka ,Ikwiriri na Kibiti waliliridhia na kuonyesha kukubali maendeleo wanayosogezewa .
Mkazi wa Mloka ,mzee Mbonde ,alisema alikuwepo enzi za hayati baba wa taifa mradi ulipofanyiwa tathmini na wa Norway.
Mzee Mbonde na bibi Fatuma Majengo walimpongeza mh rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kwa kubeba mzigo .
Walisema kwa mwanzo huu ,Dk.Magufuli atatatua tatizo la uhaba wa umeme.
Eneo litakalotumika
kujenga mradi ni kilometa za mraba 1,350 ambalo ni sawa na asilimia
tatu pekee ya eneo lote la pori la akiba la Selou yenye ukubwa wa km
za mraba 50,000 .
Mkuu wa pori hilo la
akiba la Selou kanda ya kaskazini (Matambwe)Lawrence Okode ,alisema
katika historia jina la Stiegler’s gorge limetokana na mjerumani
aliyefariki katika eneo hilo aliyejulikana kwa jina la Stiegler’s baada
ya boti yake kugonga jiwe kubwa na kusababisha umauti wake .
SHARE
No comments:
Post a Comment