Polisi nchini Rwanda wamesema wanamchunguza
Diane Shima Rwigara ambaye ni mkosoaji wa Rais Paul Kagame na ambaye
aliondolewa katika kinyang'anyiro cha urais mapema mwezi huu kwa
ukwepaji wa kodi na udanganyifu.
Msemaji wa polisi Theos Badege amesema maafisa wamefanya upekezi
nyumbani kwa familia ya Rwegara katika mji mkuu wa Kigali, na kukanusha
taarifa zilizosambaa mtandaoni kwamba amekamatwa. Badege anasema
"Rwigara hayuko chini ya ulinzi wa polisi. Kinachoendelea ni uchunguzi
juu ya mashtaka mawili. Moja ni udanganyifu unaohusishwa moja kwa moja
na Diane Rwigara binafsi na mwingine ni kukwepa kodi ambayo inahusu
familia. Jana tulifanya upekezi ulioruhusiwa kwa kibali kilichotolewa na
waendesha mashtaka lakini pia waliitwa kwa ajili ya kuhojiwa polisi.
Baadhi ya vifaa vyao vya kielektroniki kama wao kama simu na kompyuta
viko mikononi mwa polisi."Rwigara mwenye miaka 35 ambaye ni mhasibu wa zamani amemshutumu mara kwa mara Kagame kwa udhalilishaji mbaya na kukosoa chama chake cha Rwanda Patriotic Front kwa kung'ang'ania madaraka.
Tume ya uchaguzi ilimuondoa Diane katika kinyang'anyiro cha urais wa mwezi huu, ikisema kwamba hakuwasilisha saini za wafuasi wake za kutosha na kwamba baadhi ya majina aliyotuma yalikuwa ya watu waliokufa, madai ambayo aliyakanusha.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani na Umoja wa Ulaya walikosoa uamuzi huo wa kumuondoa katika mbio za urais ambazo zilishuhudia Rais Kagame akichaguliwa tena kwa asilimia 98.8 ya kura.
Polisi wamesema leo Jumatano kwamba wamefanya upekuzi katika nyumba ya Rwigara baada ya kupokea nyaraka kutoka kwa tume ya uchaguzi hata hivyo hawakutoa taarifa za kina.
Simu ya Rwigara na za ndugu zake watatu zilikuwa zimezimwa siku ya leo Jumatano wakati mwandishi wa shirika la habari la Reuters lilipojaribu kuwapigia. Mwandishi wa Reuters alipojaribu kwenda nyumbani kwa mwanamke huyo hakuna aliyefungua mlango.
Msemaji wa polisi anasema madai ya ukwepaji wa kodi yanachunguzwa kwa ushirikiano na mamlaka ya kodi nchini Rwanda.
Kamishina wa mamlaka hiyo Richard Tusabe amesema kampuni ya tumbaku ya familia ya Rwigare haijalipa kodi kwa kipindi cha miaka mitano. Hakuna ndugu wa familia aliyepatikana kuthibitisha taarifa hizo.
Kagame amepata sifa kimataifa kwa kurejesha uchumi nchini Rwanda tangu mauaji ya kimbari yam waka 1994, wakati watu 800,000 wengi wakiwa Watusi na wachache wahutu walipouawa.
Lakini pia amepata ukosoaji mkubwa kwa kile makundi ya haki za binadamu yanasema ni kuenea kwa ukiukwaji, mbinyo kwa vyombo vy ahabari vya binafsi na ukandamizaji wa upinzani.
Rwigara ni binti wa hayati Assinapol Rwigara, ambaye alianguka dhidi ya Kagame kabla ya kifo chake katika ajali ya gari mwaka 2015. Kagame amekuwa rais wa Rwanda tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari ya 1994 .
CHANZO: DW
4x4
TANZANIA YATAJWA KWENYE ORODHA YA NCHI ZENYE MISHAHARA MIKUBWA AFRIKA
Shirika la Numbeo limetoa orodha ya nchi kumi zenye mishahara mikubwa
zaidi barani Afrika. Hili ni shirika kubwa zaidi duniani la ukusanyaji
wa taarifa za majiji na nchi. Shirika hili linatoa taarifa za mara kwa
mara kuhusu hali za maisha duniani ikiwemo gharama za maisha,
upatikanaji wa nyumba za kupanga, huduma za afya, foleni za barabarani,
uhalifu na kiwango cha uchafuzi wa mazingira.
Zifuatazo ni nchi kumi za kiafrika zenye viwango vya juu zaidi vya
mshahara:
1. Libya
Libya ndiyo nchi inayoongoza barani Afrika kwa kuwa na viwango vikubwa
vya mishahara. Nchi hii yenye utajiri wa mafuta imejulikana kwa zaidi ya
miongo minne ya utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati Muammar
Gaddafi na machafuko yaliyofata baada ya kifo chake. Na pamoja kwa
machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo mpaka sasa
yanayosababisha hali ya usalama kuwa tete, kiwango cha kawaida cha
mshahara kwa mwezi baada ya makato ya kodi ni shilingi milioni tatu na
laki nane (3,800,000)
Ingawa machafuko nchini Libya yamekuwa ni kikwazo kikubwa barani Afrika,
kiwango cha hifadhi ya mafuta kwenye nchi hiyo kinachokadiriwa kuwa
mapipa bilioni 48 kunaifanya nchi hiyo sio tu kuwa moja ya nchi kumi
zenye utajiri mkubwa zaidi wa mafuta duniani lakini pia Serikali yake
inawafurahisha wananchi kwa kuwapa viwango vya juu vya mishahara pamoja
na kufanya gharama za maisha kuwa chini.
2. Zambia
Jambo kubwa zaidi litakalokufanya uhamie kwenye nchi hii isiyo na bahari
ni idadi kubwa ya wanyamapori. Ina mbuga na hifadhi nyingi sana, jambo
linaloweza kuwa la kuvutia sana kama moja ya vitu unavyopendelea ni
kufanya safari za mbugani. Kiwango cha kawaida cha mshahara kwa mwezi
nchini Zambia ni shilingi milioni tatu na laki tatu (3,300,000), na kwa
hakika huu ni mshahara mkubwa kwa yeyote yule. Gharama za kodi za nyumba
na maisha kwa ujumla nchini Zambia zipo chini. Pamoja na viwango
vikubwa kiasi hiki, Zambia kwa sasa inapitia katika mgogoro wa kisiasa
na mifumo yake ya kiuchumi na kisheria bado inafata mfumo wa uendeshaji
wa kikoloni.
3. Afrika Kusini
Mwisho wa siku kila mmoja anataka kazi yenye mshahara mzuri. Nchini
Afrika Kusini, kazi zinazotokana na taaluma za Sheria, Umeneja wa mifumo
ya kompyuta na teknolojia, waongoza ndege, udhibiti wa mafuta ya
petroli, uhandisi wa majengo na uhandisi wa programu ni baadhi ya ajira
zenye mishahara mizuri zaidi nchini humo. Kiwango cha kawaida cha
mshahara nchini humo ni shilingi milioni mbili na laki sita
(2,600,000+), ingawa wazungu bado mpaka sasa wanaishi maisha mazuri
zaidi.
4. Namibia
Uchumi wa Namibia unaendeshwa na sekta ya madini – kuchimba, kusafisha
na kusafirisha kwenda nje ya nchi. Sekta ya madini inachangia asilimia
11.5 ya pato la Taifa lakini inaiingizia nchi hiyo zaidi ya asilimia 50
ya fedha za kigeni.
Pia, Namibia ni moja ya nchi tano zinazozalisha madini ya uranium kwa
wingi zaidi na pia wana utajiri mkubwa sana wa madini ya almasi. Ingawa
uchumi wa nchi hiyo unaathiriwa sana na kupanda na kushuka kwa soko la
dunia pamoja na ukame unaoikumba mara kwa mara, mshahara wa kawaida kwa
wafanyakazi nchini humo ni shilingi milioni moja na laki sita
(1,600,000) kwa mwezi.
5. Mauritius
Nchi hii ambacho ni kisiwa kilichopo nje kidogo ya pwani ya
Kusini-Mashariki mwa Afrika kina historia ndefu ya kuwa na utulivu wa
kisiasa, utawala bora pamoja na uwajibikaji wa uwazi wa Serikali yake.
Ni moja ya nchi za Afrika zenye uchumi mzuri zaidi ikiwa na idadi ya
watu milioni 1.3. Mshahara wa kawaida nchini Mauritius ni shilingi
milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa mwezi.
6. Tanzania
Hii ni nchi ya sita kwa nchi za bara la Afrika zenye viwango vya juu vya
mshahara ambapo mshahara wa kawaida kwa wafanyakazi unakadiriwa kuwa ni
shilingi laki tisa (900,000). Zaidi ya nusu ya wafanyakazi nchini
Tanzania wapo kwenye sekta ya kilimo kama njia kuu ya kuwasingizia
kipato. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Tanzania imeweza kuwa na uchumi
imara na unaokua kwa asilimia saba kila mwaka katika kipindi cha miaka
kumi iliyopita. Kiwango cha umaskini kimeendelea kupungua na vita dhidi
ya Rushwa inayoongozwa na Rais John Magufuli inabaki kuwa msingi imara
wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
7. Morocco
Tangu mwezi Oktoba mwaka 2016 nchi ya Morocco imekuwa kwenye mgogoro
mkubwa sana wa kisiasa. Kwa sasa, nchi hiyo ina muunganiko mkubwa wa
vyama vya siasa unaojumuisha vyama sita vya siasa nchini humo. Kilimo
bado kinachangia asilimia 15 ya pato la Taifa. Pamoja na nchi hiyo
kukumbwa na ukame mkubwa mwaka 2016, bado waliweza kuweka rekodi ya
mavuno mengi zaidi ya nafaka. Katika nchi ya Morocco, mshahara wa
kawaida kwa wafanyakazi ni shilingi laki tisa (900,000).
8. Zimbabwe
Mshahara wa kawaida kwa wafanyakazi nchini Zimbabwe ni shilingi laki
nane (800,000). Nchi hii inayoongozwa na Rais Robert Mugabe tangu kupata
kwa uhuru wake inatabiriwa kuwa itaweza kuwa na uchumi bora zaidi ya
sasa na kupunguza umaskini iwapo itadhibiti hali ya kisiasa na kufikia
makubaliano kuhusu kufanyika kwa siasa na sera za ushindani kwenye
uwekezaji.
9. Ghana
Nchi hii imepiga hatua kubwa sana kwenye kujenga demokrasia imara. Ni
nchi inayosifika kwa kuwa na mfumo huru wa Mahakama pamoja na uhuru wa
vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza kwa wananchi na wanaharakati.
Mshahara wa kawaida nchini Ghana ni shilingi laki saba (700,000) kwa
mwezi. Uchumi wa nchi hii unategemea zaidi sekta ya mafuta, sekta
nyingine zisizo za mafuta zina mchango mdogo kwenye uchumi wa nchi hiyo.
10. Algeria
Pamoja na bei ya mafuta kuporomoka kwenye soka la dunia, bado uchumi wa
Algeria uliweza kukua kwa asilimia 3.8 mwaka 2016 ingawa pia yategemewa
uchumi wake utashuka kati ya mwaka 2017 na 2019. Kiwango cha kawaida cha
mshahara nchini Algeria baada ya makato ya kodi ni shilingi laki sita
na elfu hamsini (650,000), kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na
nchi nyingine nyingi za Afrika.
About Richard Mwaikenda
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
SHARE
No comments:
Post a Comment