Afisa
wa Ubalozi wa Marekani anayeshughulikia masuala ya umma Bi. Brinille
Ellis aliwakaribisha wanafunzi, wazazi na walimu zaidi ya 100 katika
Shule ya JOMAK School iliyopo huko Bahari Beach katika mahafali ya
washiriki wa programu ya mafunzo ya Kiingereza inayofadhiliwa na Ubalozi
iitwayo “English Access Microscholarship Program”.
Wanafunzi
wapatao 25 wa vidato vya tatu, nne na tano walianza kuhudhuria mafunzo
yao ya Kiingereza baada ya masomo ya kawaida shuleni katika shule ya
JOMAK hapo mwezi Septemba mwaka 2015. Hawa watakuwa kundi la kwanza la
wahitimu wa programu hii jijini Dar es Salaam. Serikali ya Marekani
inafadhili madarasa mengine matatu hapa nchini chini ya programu hii.
Hii ni pamoja na darasa la pili katika shule ya JOMAK na madarasa
mawili mjini Moshi yanayoendeshwa na taasisi iitwayo Kilimanjaro
Information Technology. Inatarajiwa kuwa madarasa mengine yataanza mwezi
Januari 2018 katika miji ya Mwanza, Tanga and Zanzibar.
Bi.
Ellis aliwapongeza wanafunzi wa programu hii kwa kujitoa kwao kwa dhati
na kushiriki kikamilifu katika mafunzo yao: “Kwa kupitia programu ya
Access mmepata mambo mengi zaidi ya ujuzi wa lugha ya Kiingereza.
Mmekuwa viongozi wa jamii na mfano wa kuigwa katika jamii zenu.” Wakati
wa hafla hii, wanafunzi walifanya maonyesho na kutambulisha kwa
Kiingereza miradi na kazi mbalimbali za kuhudumia jamii walizozifanya
wakati wa mafunzo yao katika programu hii.
Programu
ya Access hutoa mafunzo ya msingi ya lugha ya Kiingereza kwa watoto na
vijana wenye vipaji wa kuanzia miaka 13 hadi 20 kutoka jamii zenye hali
duni kiuchumi kupitia madarasa yanayoendeshwa baada ya muda wa shule na
yanayotoa mafunzo ya kina. Programu ya Access huwapatia washiriki wake
stadi za lugha ya Kiingereza jambo ambalo huwapa fursa zaidi za kielimu
na ajira. Toka mwaka 2004, zaidi ya wanafunzi 200 kutoka Tanzania na
100,000 kutoka zaidi ya nchi 85 wameshiriki katika programu hii.
SHARE
No comments:
Post a Comment