TRA

TRA

Wednesday, September 6, 2017

WASAFIRI KUTOKA INDIA HADI MAREKANI KUMPIGA MKWE WAO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
                      Wanandoa wawili wenye asili ya India Jasbir mwenye mika 67 na mkewe Bhupinder Kalsi mwenye miaka 61 pamoja na mtoto wao wa kiume Devbir Kalsi mwenye umri wa miaka 33, wanashikiliwa na Polisi Marekani baada ya wanandoa hao kusafiri kutoka India hadi Florida, Marekani kwa lengo la kumpiga mke wa mtoto wao huyo kwa sababu si mtiifu kwao.

Mwanamke huyo anayeitwa Silky Gaind, 33, alipiga simu kwa wazazi wake walioko India na Polisi kuwajulisha kuwa amefungiwa ndani na anapigwa na mumewe na wakwe zake ndipo Polisi walipofika eneo hilo kumwokoa ambapo alikuwa anapigwa akiwa na mtoto wake.

Kwa mujibu wa Polisi walipofika eneo hilo walikuta mlango umefungwa na kuamua kuuvunja na walipoingia ndani waliwakuta watatu hao wakimshambulia mwanamke huyo huku taarifa zikieleza kuwa ni tabia ya mwanamme huyo kumpiga mkewe na wakati huu akaamua kuomba msaada wa wazazi wake.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger