MBUNGE wa
jimbo la Kibiti ,mkoani Pwani Ally Ung’ando wa katikati akiwa kwenye
ziara yake ya jimbo ya siku 21 ambayo ameianza katika kata ya Rualuke
MBUNGE wa
jimbo la Kibiti ,mkoani Pwani Ally Ung’ando akizungumza na wakazi wa
vijiji vilivyopo kata ya Rualuke wakati wa ziara yake ya jimbo ya siku
21 ambayo ameianza katika kata ya hiyo.Picha na Mwamvua Mwinyi
Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti
MBUNGE wa
jimbo la Kibiti mkoani Pwani ,Ally Ung’ando amewataka wananchi jimboni
hapo kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa
kujishughulisha kimaendeleo ili kupiga hatua kiuchumi.
Amewaomba
kushirikiana kwenye miradi ya maendeleo badala ya kuiachia serikali ama
viongozi pekee suala ambalo linakwamisha jitihada mbalimbali
zinazoendelezwa.Ung’ando aliyasema hayo kijiji cha Rungungu kata ya
Rualuke katika ziara yake ya siku ya kwanza aliyoianza kwenye kata hiyo
ambapo anatarajia kuendelea na ziara hiyo kwa siku 21 katika kata Tisa
na vijiji vyote jimboni hapo.
Aliwataka
vijana kuacha kujisahau kufanya kazi na kujiunga vikundi ili waweze
kuwezeshwa kirahisi.“Vijana mjitume ,acheni kuishi kimazoea kwani
maendeleo yoyote yanaletwa kwa kujituma ” alisema mbunge huyo.Hata hivyo
,alikemea tabia inayofanywa na baadhi ya wakulima wa korosho ambao
wanauza korosho zao kwa mfumo usio rasmi wa kangomba .
Ung’ando
alisema mfumo unaotambulika ni mfumo wa stakabadhi ghalani lakini
wakulima wamekuwa wakiuza korosho zao kiholela .“Niwaombe muache kuuza
korosho zenu kwa madalali ,hawawasaidiii,mtakuja kupata hasara na
mkumbuke serikali haitohusika na mtu anauza korosho zake kiholela,msije
kuipa lawama serikali wakati wenyewe mnataka njia nyepesi
zinazowakandamiza ” alisema.
Pamoja na
hayo ,aliwasihi wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule kupata
haki ya elimu .Ung’ando alisema serikali chini ya Rais John Magufuli
inatoa elimu bure kwa wanafunzi wa msingi hadi kidato cha nne lakini
wazazi wamekuwa wakiwanyima fursa hiyo watoto wao.Katika ziara hiyo pia
anatoa mifuko ya saruji 100 kwa kila kata,ambayo itakayosaidia kusukuma
maendeleo ya kata hizo.
Ung’ando
alianza ziara yake ya jimbo desemba 26 kwa kuzungumza na kusikiliza kero
kwa wapiga kura wake katika vijiji vya Rungungu,Kilola Tambwe na
Nyamatanga kata ya Rualuke,Ziara itaendelea desemba 28 kupisha ziara ya
naibu waziri wa Nishati Mh,Subira Mgalu ambae yupo jimbo la Kibiti kwa
ajili ya kuangalia changamoto ya nishati ya umeme .
SHARE
No comments:
Post a Comment