Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu (kulia),
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga na Dk. Mohamed Mohamed wa
ugonjwa wa Kisukari katika hospitali hiyo wakikata keki maalumu
iliyotengenezwa kwa bidhaa za Sugar Free zisizo na sukari wakati wa
uzinduzi wa bidhaa hizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.
Muonekano wa keki hiyo iliyotengenezwa kwa bidhaa hizo zisizo na sukari.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza bidhaa hizo.
Hii ndiyo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo.
Na Dotto Mwaibale
……………………………………………………………………
WANANCHI
jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake wameipongeza Kampuni ya Abacus
Pharma (A) LTD kwa kuwaletea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia
kupunguza matumizi makubwa ya sukari kwenye vyakula.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam
walisema kampuni hiyo haina budi kupongezwa kwa kuzileta bidhaa hizo
katika soko la Tanzania ili kukabiliana na changamoto ya matumizi
kupitia vyakula.
“Hivi
sasa kila pembe ya nchi yetu kumekuwa na changamoto ya ugonjwa wa
kisukari ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na mfumo wa ulaji na unywaji
wa vyakula vyenye sukari kupita kiasi kwa bidhaa hizi mpya
zinazosambazwa na Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD hakika itasaidia
sana” alisema Frank Erasto mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam.
Erasto
alisema yeye ni mihongoni mwa waathirika wa ugonjwa wa kisukari lakini
tangu bidhaa hizo ziingie katika soko la Tanzania amekuwa akitumia
bidhaa hizo ili asiongeze sukari mwilini mwake baada ya kupata matibabu.
Mkazi
wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina moaja la
Reuben alisema familia yake imeanza kutumia bidhaa hizo ambazo hazina
gharama kubwa.
“Familia
yangu na marafiki zangu tumeanza kutumia bidhaa hizi za Sugar Free
kusema kweli ni nzuri na zina radha kama ile zilizopo kwenye chakula
halisi” alisema Reuben.
Mkazi
wa Kariakoo Happyness Kimaro alisema kwake anaona bidhaa hizo ni
mkombozi kwani ameanza kuzitumia baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa
kisukari na hapendi kuongeza sukari mwilini mwake.
“Sisi
wagonjwa wa kisukari tumekuwa na changamoto kubwa ya ulaji wa vyakula
mara tunaambiwa tusile hiki na kile tule vyakula ambavyo havina sukari
ambavyo havina ladha sasa kwa kuletewa bidhaa hizi tunasema ni nafuu
kwetu” alisema Kimaro.
Akizungumza
bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD,
Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
matumizi makubwa ya sukari katika vyakula.
Alisema
bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la
sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la
nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo
zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni
shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.
“Bidhaa
hizi zipo za aina mbili za sugar free gold ambazo hutumika katika
chai, uji, na vinywaji baridi tu na sugar free natura hutumika katika
baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia
hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi
sana,” alisema Babu.
Alisema
kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi
kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa
mkubwa.
Aliongeza
kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia
jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina
ladha ya sukari kama ile ya kawaida na kwamba bidhaa hizo
zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Akizungumza
katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na
Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga
alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi
ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.
Alisema
hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama
wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya
kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika.
Aliongeza
kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya
pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji
kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika
matumizi mengine.
Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.
Akizungumzia
bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa
zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine
visivyo na sukari kupata radha ile ile.
Alisema
mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa
vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.
SHARE
No comments:
Post a Comment