Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akitia
saini katika kitabu cha wageni mara alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya Ziara ya siku mbili ya kikazi Mkoani hapo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma Dkt. Paul Chaote akitoa taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndugulile(Mb) katika Ziara ya siku mbili ya kikazi ya Naibu Waziri huyo
Mkoani hapo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb)
akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Nyanganga mara baada ya kuwasili
katika kushiriki ujenzi wa madarasa manne ya Shule ya Kijiji hicho
katika kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika kufanya shughuli za
maendeleo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya Uvinza Bw. Lutabola Weja akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa
zoezi la kuamsha ari ya wananchi kujishughulisha katika shughuli za
maendeleo ambapo wanachi wa Kijiji cha Nyanganga wamejitolea na kujenga
vyumba vinne vya madarasa kwa ajili ya shule ya Kijiji chao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb)
akishirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nyanganga kuchanganya zege kwa
ajili ya kuweka ‘rental’ kwa ajili ya madarasa manne ya Shule ya Kijiji
hicho katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika kufanya
shughuli za maendeleo.
Mtendaji wa Kjjiji cha Nyanganga
Bw.Erick Ruhomola akitoa taarifa ya Mradi wa ujenzi wa Shule ya
Sekondari ya Kijiji chao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ambao
uliibuliwa, kubainishwa na kutekelezwa wananchi wenyewe na wananchi kwa
takribani.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe.
Mwanamvua Mrindiko akimshukuru Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) kwa kuja
kuonesha mfano wa kuamsha ari ya wananchi wa Uvinza kujitolea katika
shughuli za maendeleo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb)
akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyanganga mara baada ya kushiriki
zoezi la kuamsha ari katika ujenzi wa Shule ya Kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Nyanganga
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) mara baaada ya kushirikiana
naye katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi katika ujenzi
wa vyumba vine vya madarasa ya shule ya Sekondari ya Kijiji chao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb)
akikabidhi mifuko 37 ya Saruji kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
wananchi wa Kijiji cha Nyanganga wa kujitolea kwa nguvu zao kujenga
shule ya Sekondari ya Kijiji chao.
Baadhi ya wananchi wakifanya kazi
ya kumwaga ‘rental’ katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kijiji cha
Nyanganga kilichopo Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
……………………..
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb)
ameshiriki ujenzi wa Shule ya Kijiji cha Nyanganga iliyoko kata ya
Kazuramimba, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ikiwa ni jitihada za
wananchi wa kijiji hicho kuharakisha upatikanaji wa huduma ya elimu
kijijini hapo.
Akiwa katika Kijiji hicho Naibu
Waziri Dkt. Ndugulile ameshiriki zoezi la kumimina zege kwa ajili ya
kufunga ‘rental’ ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo.
Dkt. Ndugulile amesema lengo la
kuwepo ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya
Jamii (1996), na Sera nyingine za Wizara amabzo zinasisitiza ushiriki wa
jamii katika kuibua mahitaji, kupanga, kuamua, kutekeleza, kufuatilia
na utathmini shughuli za miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa
huduma ya miundo mbinu ya kufundishia na kujifunzia katika maeneo ya
mijini na vijijini.
Mhe. Ndugulile ameongeza kuwa Ili
kurejesha ari ya wananchi kushiriki katika maendeleo yao kuelekea uchumi
wa kati na wa viwanda, Wizara imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya
Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa kwa kuhamasisha jamii kushiriki na kuchangia shughuli
za maendeleo yao kwa kufanya kazi za bega kwa bega, kuchangia nguvu zao,
rasilimali fedha, rasilimali vifaa na ufundi kwenye utekelezaji wa
miradi ya ujenzi wa miundo ya elimu, afya, kilimo, mifugo, barabara na
viwanda vidogo vidogo.
“Nimeambiwa kuwa mradi wenu wa
ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji cha Nyanganga utasaidia
kusogeza huduma ya elimu jirani na wananchi, na nimevutiwa na hamasa
mliyonayo katika maendeleo name nimekuja kushirikiana nanyi kuendeleza
ujenzi wa madarasa ya shule kazi amabyo ni kigezo thabiti cha cha
dhamira ya dhati yawananachi wa kijiji hiki katika kutoa haki ya msingi
ya kumwendeleza Mtoto katika ngazi ya kijiji na jamii kwa ujumla”
alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kjjiji
cha Nyanganga Bw.Erick Ruhomola amesema kuwa Mradi wa ujenzi wa Shule
ya Sekondari ya kijiji uliibuliwa na kubainishwa na wananchi wenyewe na
kutekelezwa na wananchi kwa takribani asilimia mia moja hadi kufikia
hatua ya kumwaga zege kwa ajili ya ‘rental’.
“Tunaishukuru Serikali kwa
kutuona na kuja kutuunga mkono katika jitihada zetu za kujiletea
maendeleo katika kijiji chetu” alisisitiza Bw. Ruhomola.
Naye Mkuu wa Wilaya yaUvinza Mhe.
Mwanamvua Mrindiko amemshukuru Naibu Waziri kwa kuja kuonesha mfano wa
kuamsha ari ya wananchi wa Uvinza kujitolea katika shughuli za maendeleo
yao.
“ Hili ni Jambo la kipekee kwa
Mhe. Naibu Waziri kutembelea na kushiriki na wananchi katika ujenzi wa
shule hii” alisisitiza Mhe.Mwnanamvua
Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya
Kijiji cha Nyanganga kilichopo Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma
itawasaidia watoto wa jamii hiyo kuwa na shule karibu na makazi yao
ambapo hapo awali watoto hao walikuwa wanatembea umbali wa kilometa 14
kwenda shule ya jirani.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile yupo katika
Mkoa wa Kigoma kwa ziara ya siku mbili ya kikazi kufuatilia utekelezaji
wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na Wizara yake.
SHARE
No comments:
Post a Comment