BEKI
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Juma ‘Chama’ aliyeweika
klabu za Pamba FC ya Mwanza na Yanga ya Dar es Salaam amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa
amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Kiharusi.
Chama
ni jina la utani ambalo marehemu Athumani Juma alipewa kutokana na beki
wa zamani wa kimataifa wa Zambia, Dick Chama ambaye naye ni marehemu
aliyecheza kwa mafanikio timu ya taifa ya kwao kwa kipindi cha miaka 10
kuanzia 1967 hadi 1976 na klabu za za Mufulira Wanderers, Green
Buffaloes na Bancroft Blades.
Athumani
alipewa jina hilo baada ya kujiunga na Yanga SC mwaka 1981 akitokea
Pamba ya Mwanza na mashabiki wa timu hiyo ya Jangwani walimbatiza Juma
jina hilo baada ya beki wao mwingine, Rashid Idd aliyekuwa akiitwa Chama
pia kuhamia Pan Africans baada ya kudumu tangu Jangwani tangu 1979.
Na
umaarufu wake zaidi Jangwani ukaja kutokana na alivyoweza kumdhibiti
mshambuliaji hatari wa mahasimu enzi hizo, Simba SC, Zamoyoni Mogela
‘Golden Boy’.
Kisoka,
Chama aliibukia Pamba FC ya Mwanza alikozaliwa na kukulia kabla ya
kujiunga na Yanga SC na aliocheza nao wakati huo ni akina Joseph Fungo,
Yussuf Ismail Bana, Ahmed Amasha ‘Mathematician’, Isihaka Hassan Chukwu,
Juma Mukambi ‘Jenerali’, Hussein Iddi, Charles Boniface Mkwasa, Abeid
Mziba ‘JJ Masiga’, Elisha John, Ali Mchumila, Makumbi Juma ‘Homa ya
jiji’, Omar Hussein ‘Keegan’, Juma Kampala na wengineo.
Chama
pia alikuwa akijulikana kwa jina lingine la utani, Jogoo ambalo alipewa
mwaka 1981 kwenye michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya kutokana na
mchezaji mmoja wa Harambee Stars, Sammy Onyango ‘Jogoo’.
Chama
alistaafu soka mwaka 1990 na kujikita kwenye biashara zake ndogo ndogo
kabla ya kuanza kusumbuliwa na maradhi mwaka 2014 na kujikuta anashindwa
kufanya shughuli yake hadi umauti wake.
Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Chama. Amin.
SHARE
No comments:
Post a Comment