TRA

TRA

Thursday, February 25, 2016

KLABU YA KIMATAIFA LIONS CLUB INTERNATIONAL YATOA MSAADA WA MADAWATI YA CHUMA SHINYANGA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Leo Februari 24,2016 ,Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani kimetoa msaada wa madawati 165 yenye thamani ya shilingi milioni 18 katika shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga ili kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa chini.
Pichani viongozi wa wilaya ya Shinyanga,wazazi na maafisa kutoka Lions Club International wakiongozwa na Gavana wa Lions Club katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini bwana Hyderali Gangji wakiwa katika shule ya msingi Town…Madawati hayo 165 yametolewa na Lions Club ya mkoa wa Mwanza.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama  Malunde ametuletea picha 30 kilichojiri mwanzo hadi mwisho
Hapa ni katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(katikati).Kushoto ni meya wa manispaa ya Shinyanga,ambaye pia ni diwani wa kata ya Shinyanga ilipo Shule ya Msingi Town na Mwenge akimtambulisha gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji na jinsi klabu hiyo inajihusisha na utoaji wa misaada kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji
Wanachama wa Lions Club International walioambatana na gavana
Kulia ni gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji akieleza namna klabu yake inavyofanya kazi katika nchi 210 duniani kote
Wanachama wa Lions Club International wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema Lions Club International ina wanachama Milioni 1 na laki nne duniani kote na nchini Tanzania kuna vilabu 18 na nchini Uganda vilabu 24
Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali mkoani Shinyanga ambapo mwaka jana walitoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata wilayani Kahama,pia chakula katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija,kutoa madawati katika shule ya msingi Town na Mwenge

Miongoni mwa madawati ya chuma 165 yaliyotolewa na Lions Club International katika shule ya msingi Town na Mwenge katika manispaa ya Shinyanga
Hapa ni katika shule ya msingi Town katika manispaa ya Shinyanga ,aliyesimama ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Said Juma Issa akiwakaribisha viongozi mbalimbali waliofika katika shule wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati 65 kwa shule hiyo na 100 katika shule ya msingi Mwenge

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Town wakiangalia madawati waliyopewa na Lions Club International 
Kulia ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini,ambaye pia ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam aliyefanya jitihada za kupatikana kwa madawati katika shule za kata yake,Town na Mwenge.Diwani huyo pia ni mwanachama wa Lions Club International
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Town Josephine Mabula akisoma risala kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambapo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 1104 sasa haina uhaba tena wa madawati baada ya kupokea kutokaLions Club International

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger