Aliyewahi kuwa
kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amejiunga na timu ya taifa ya
Trinidad na Tobago, Shirikisho la Soka la nchi hiyo limemtangaza mjini
Port of Spain.
Saintfiet
anayechukua Stephen Hart aliyefukuzwa,amesaini mkataba wa miaka miwili,
wakati Carolina Morace wa Italia anachukua majukumu ya timu ya taifa ya
wanawake.
Huku
T&T kwa sasa ikishiriki hatua ya mwisho ya mchujo wa kufuzu Kombe la
Dunia kwa CONCACAF na ikiwa haina hata pointi moja baada ya mechi
mbili, ujio wa Saintfiet unaweza kuinua kiwango cha timu na kupata
matokeo mazuri katika mechi mbili zijazo za ugenini na Panama Machi 24
na Mexico Machi 28.
Rais wa
TTFA, David John Williams alisema: “Kama hatapata matokeo mazuri katika
mechi mbili zijazo tutamfukuza kwa sababu tutakuwa tumetolewa kwenye
mbio za kuwania tiketi ya Kombe la Dunia tusipopata matokeo mazuri,”.
Saintfiet,
mwenye umri wa miaka 43, alichezea vigogo wa Ubelgiji enzi zake, FC
Boom kuanzia mwaka 1983 hadi 1997 kabla ya kuwa kocha akiwa ana umri wa
miaka 24, akiweka rekodi ya kocha kijana zaidi kuwahi kutokea katika
soka ya Ubelgiji.
Pamoja na
Yanga aliowaachia Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka
2012 baada ya miezi miwili ya kuwa kazini, pia amefundisha timu nyingine
nyingi zikiwemo klabu na za taifa katika nchi za Ujerumani, Finland,
Jordan, Qatar, Ubelgiji, Uholanzi, Zimbabwe, Ethiopia and Namibia, Togo
na Bangladesh.
Kwa
upande wake, Carolina Morace mwenye umri wa miaka 52 ni mshambuliaji wa
zamani wa timu ya taifa ya Italia ambaye pia amechezea klabu mbalimbali
za wanawake Serie A na alikuwa mfungaji bora katika michuano ya nyumbani
kwao msimu wa 1984-1985, kabla ya kuendeleza makali yake kuanzia msimu
wa 1987-1988 hadi 1997-1998.
Baada ya
kustaafu akaanza ukocha Lazio kabla ya kufundisha timu timu ya taifa ya
wanawake ya I]talia kuanzia 2000 hadi 2005, na timu ya taifa ya wanawake
ya Canada kuanzia mwaka 2009 hadi 2011.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment