Picha
ya juu na chini ,Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Wadau wa Maendeleo na
viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ofisini kwake mjini
Unguja.
Picha ya pamoja
Balozi
Seif Ali Idd akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus
Mwamanga baada ya kupata maelezo ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo
kisiwani Zanzibar,anayewaangalia ni Msimamizi wa shughuli za TASAF
katika Benki ya Dunia ,Bwana Muderis Mohamed.
Mmoja
wa wanafunzi wa shule ya Msingi Kizimbani,Unguja ambaye anatoka kwenye
Kaya ya Mlengwa Wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini akikokotoa hesabu,
anayemwangalia ni Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia
Bwana Muderis Mohamed.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga(aliyesimama)akizungumza na
baadhi ya wananfunzi wanaotoka katika Kaya za Walengwa wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Masikini katika shule ya msingi Kizimbani kisiwani
Zanzibar.
Msimamizi
wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia akiwa katika picha na baadhi
ya kununua kikapu kilichotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Masikini huko Kizimbani, kisiwani Zanzibar. Nyuma yake ni bidhaa
zilizotengenezwa na walengwa hao kama njia mojawapo ya kujiongezea
kipato.
NA Estom Sanga- Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi
amesema mchango unaotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika
kuhamasisha wananchi kupambana na umasikini unapaswa kuungwa mkono kwani
unakwenda sambamba na dhamira ya serikali zote mbili za kuwaondolea
wananchi kero ya umasikini.
Balozi
Iddi ametoa kauli hiyo alipokutana na baadhi ya wadau wa Maendeleo na
Maafisa wa TASAF ofisini kwake mjini Unguja baada ya viongozi na wadau
hao wa maendeleo kuhitimisha ziara ya kuwatembelea Walengwa wa Mpango wa
Kunusuru Kaya masikini kisiwani humo.
Amesema
mafanikio makubwa yanayojitokeza katika nyanja za elimu, afya na
ongezeko la shughuli za kiuchumi miongoni mwa walengwa wa Mpango huo ni
ushahidi tosha kuwa wananchi hususani wale ambao wamekuwa wakikabiliwa
na umasikini , wanahitaji kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa shughuli za
Mpango huo ambao umekuja kwa wakati hasa kutokana na ukubwa wa tatizo
la umasikini nchini.
Balozi
Iddi amesema kwa kutambua hilo serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itaendelea kuunga mkono utekelezaji wa shughuli za TASAF kisiwani humo
na kuwataka wananchi hususani wale walioko kwenye Mpango wa kunusuru
kaya masikini kutumia fursa hiyo vizuri ili hatimaye waweze kuboresha
maisha yao.
Akizungumza
katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga
amesema hatua zilizochukuliwa na serikali katika kuweka msukumo wa
kutosha katika utekelezaji wa Mpango huo zimeendelea kuzaa matunda
ambapo katika maeneo mengi nchini kote walengwa wameonyesha kuanza
kubadilika kwa kuboresha maisha hususani katika nyanja za makazi, elimu,
afya na kuunda vikundi vya kuweka akiba na vya uzalishaji mali.
Kwa
Upande wake Msimamizi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia,Bwana
Muderis Mohamed, amesema wadau wa maendeleo wameonyesha kuridhishwa na
matokeo mazuri yaliyoanza kuonekana kwa kaya za walengwa wa Mpango wa
Kunusuru kaya masikini jambo linaloendelea kuwavutia wadau wengi
kujitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya Mpango huo.
Serikali
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF inaendesha Mpango wa Kunusuru
Kaya Masikini nchini kote ambapo takribani kaya MILIONI MOJA NA LAKI
MOJA zinazokadiriwa kuwa na wakazi takribani walengwa milioni SITA
zinanufaika na mpango huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment