Mwandishi Wetu, Korogwe
MBUNGE wa Korogwe Vijijini, Stephen
Ngonyani 'Profesa Majimarefu' amemwomba Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Stella Manyanya kumwongezea nguvu ili kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa
ya Sekondari ya Mazinde wilayani humo.
Mbunge Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani
Majimarefu aliwasilisha ombi hilo
kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi akitaka jamii
kuungwa mkono katika kumalizia kazi ya ujenzi madarasa iliyoanza.
Alisema wananchi kwa kushirikiana na
mkuu wa wilaya hiyo wamefanya kazi kubwa kufanikisha ujenzi wa vyumba viwili, wakijitolea
rasilimali zao ikiwemo nguvu kazi.
Majimarefu alisema katika kuthamini
mchango wa wananchi iko haja kwa Serikali kupitia wizara ya elimu kuunga mkono
jitihada zilizoanza kuoneshwa kwenye eneo hilo.
"Dada yangu, Naibu Waziri Stella Manyanya, niseme kazi
umeiona, sasa nikuombe najua utasema kitu hebu ona namna ya kutusaidia hapa,"
alisema.
Licha ya kuyasema hayo, mbunge huyo
alimmwagia sifa DC wa Korogwe, Robert Gabriel kwa utendaji kazi wake wenye
ubunifu uliowezesha kutekelezwa miradi mbalimbali ya ujenzi yakiwemo madarasa.
Gabriel alimhakikishia kiongozi huyo
kuwa, fedha itakayolpelekwa kwa ajili ya miradi itakuwa salama na kutumika kama
ilivyokusudiwa.
Stella alisema wazazi wana jukumu la
kuendelea kishirikiana na Serikali yao kufanikisha miradi mbalimbali ya
maendeleo, hasa ujenzi wa madarasa.
Alisema inasikitisha kuona wazazi
wanashindwa kukarabati madarasa yaliyopo, huku wakimudu kuwapeleka watoto wao
shule za kulipia, lakini kama wangekuwa na ushirikiano mambo makubwa kwa maslahi ya jamii
yangeweza kupatikana.
Naibu Waziri huyo alikemea tabia za
wazazi kuwaoza watoto wao na vitendo vya mimba dhidi ya watoto ambavyo huchangia
kukwamisha vijana kutimiza ndoto za maisha.
Akijibu maombi ya Profesa Majimarefu,
Naibu waziri aliwaomba wananchi wa Mkomazi kuendelea kukamilisha kazi
waliyoianza, huku akiahidi wizara kusaidia kukamilisha jitihada hizo.
Alisema atahangaika huku na huko
hadi kuhakikisha na kwamba atawawezesha wananchi wa Mazinde kujenga vyumba
vingine viwili vya madarasa vitakavyoondoa changamoto iliyopo.
ciao
SHARE
No comments:
Post a Comment