BENKI ya CRDB imetoa msaada wa viti
20 kwa ajili ya maabara ya Shule ya sekondari ya Kiwanja iliyopo wilayani Chunya
Mkoa wa Mbeya.
Wakipokea msaada huo wakazi na
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kiwanja wameishukuru benki ya CRDB kwa kuwasaidia viti 20 kwa ajili ya chumba cha
Maabara.
Akitoa msaada huo Meneja wa Benki
hiyo tawi la Chunya Hamisi Mbinga alisema katika kutoa mchango kwa jamii
wanayoizunguka na kuendeleza elimu waliamua kujitolea kwenye swala la maabara
ili wanafunzi wa shule hiyo waweze kujifunza kwenye mazingira yaliyo bora.
Aliendeleza kueleza kuwa wao kama
sehemu ya jamii wamekuwa wakishirikiana na wakazi wa chunya ambapo mbali na
kutoa viti hivyo pia wameweza kuchangia kwenye sekta ya michezo kwa kutoa
kwa kiasi cha fedha cha shilingi laki nne.
Alisema laki mbili zilikwenda
Halmashauri kwa ajili ya kuchangia Michezo na laki mbili zilitumika katika ligi
ya wilaya ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la kinawiro cup ambayo
ilitumika kununua mipira.
Wakiongea kwa nyakati tofauti
wakazi wa wilaya ya Chunya Jeremia Zakaria na Pasto Joshua walisema kwa kipindi
kifupi toka tasisi hiyo ya crdb ianze kufanya huduma zake za kifedha
wilayani hapo wamekuwa wakishirikiana vizuri na benki hiyo kwa ukaribu
kwenye maswala ya maendeleo na kufanya wilaya ya chunya izidi kukua
kimaendeleo.
Mwisho.
SHARE








No comments:
Post a Comment