RAIS Dk.
John Magufuli ameendelea kutumbua majipu baada ya kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu pamoja na wasaidizi wake wanne.
Pia, ameagiza
vyombo mbalimbali kufanya uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili viongozi hao wa
Nida.
Hayo
yalisemwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na
waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Balozi Sefue
alisema Rais Magufuli amefikia uamuzi huo kutokana na taarifa za mamlaka hiyo
kuonesha wamepokea fedha nyingi, lakini wameandikisha wananchi wachache kupata
vitambulisho vya taifa.
Alisema
pamoja na Maimu, Rais ametungua pia uteuzi wa Mkurugenzi wa Teknolojia Habari
na Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni, Ofisa
Ugavi Mkuu, Rahel Mapande na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.
Sefue
alisema taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa hadi sasa Nida imetumia sh.
bilioni 179.6 kiasi ambacho ni kikubwa hivyo angependa kufanyike uchunguzi na
ukaguzi ili kujua namna fedha hizo zilivyotumika.
SHARE









No comments:
Post a Comment