TRA

TRA

Saturday, January 23, 2016

Serikali ya mpito Sudan Kusini kutoanza kama ilivyopangwa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


 
Serikali ya mpito ya Sudan Kusini iliyotarajiwa kuanza rasmi shughuli zake hii leo imetangaza kuakhirisha mpango huo.
Msemaji wa serikali Atenya Wek Ateny, amethibitisha hayo na ameweka wazi kwamba takriban thuluthi mbili ya masuala ya kiserikali yataendeshwa kama ilivyokuwa huko nyuma. Serikali hiyo ya mpito ya Umoja wa Kitaifa ilitarajiwa kuundwa leo (22.01.2016) ili kumaliza mgogoro wa miaka miwili uliosababisha zaidi ya watu 15,000 kuuwawa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Serikali ya mpito ya Umoja wa Kitaifa ilikuwa ikitarajiwa kuundwa na kuanza kazi leo ikihusisha mawaziri 30.
Kuundwa kwa serikali hiyo ni mchakato uliokwenda sambamba na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini na viongozi wawili wanaozozana Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar kufuatia shinikizo la kimataifa mnamo mwezi Agosti mwaka jana.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha watu zaidi ya milioni mbili kuachawa bila makaazi vilihusisha mapambano kati ya wanajeshi wa serikali ya Rais Kiir na waasi wanaomuunga mkono mpinzani wake kisiasa Riek Machar.
Siku ya kihistoria
Kimsingi leo ilikuwa siku muhimu iliyotarajiwa kuweka msingi wa kupigwa hatua katika historia ya taifa hilo la Sudan Kusini ambalo limeshuhudia miaka miwili ya mapigano kati ya pande hizo mbili hasimu.
Raia zaidi ya milioni 12 wa nchi hiyo walitarajia kuiona serikali mpya ya mpito itakayozijumuisha pande zote huku Salva Kiir akiendelea kushikilia nafasi yake kama rais na Machar kurudishwa katika nafasi yake ya zamani, yaani makamu wa rais.
Serikali hiyo ya mawaziri 30 ikitarajiwa kwamba itajumuisha watu sita walioteuliwa na Rais Kiir huku wengine 10 wakiteuliwa na Machar na wawili wakiteuliwa kutoka upande wa wale waliokuwa wamezuiliwa jela na wengine wawili wakiteuliwa na muungano wa vyama vidogo vya kisiasa nchini Sudan Kusini.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger