MARA nyingi katika jamii kumekuwepo na neno
linalotumiwa la ‘presha’ likiwa na maana wasiwasi na kutojiamini. Na hii
imekuwa ikitumika pale mtu anapokabiliwa na wakati mgumu kwa jambo fulani.
Sawia na matumizi hayo, kuna pia
wanaoelezewa kuwa wanaugua presha na wanatumia dawa. Namna neno hilo
linavyotumiaka yawezekana likawa linasababisha utata.
Hata
hivyo, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha
Utafiti Tukuyu mkoani Mbeya inaeleza kwamba unapozungumzia kuhusu presha
unaimanisha shinikizo la damu au wengine hufupisha kwa neno ‘BP’, ikiwa ni
kifupi cha maneno ya kiingereza ya ‘Blood Presure.’
Moyo
Maana ya Shinikizo la damu
NIMR inasema kuwa shinikizo la damu au presha ni kipimo cha damu ambacho kinapima
nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo ukidunda.
Kwa kawaida mtu anapopimwa huainishwa kwa vipimo
viwili; presha ya systole na diastole.
Systole ni kipimo cha juu mfano 140 mm Hg ambacho
hupima nguvu ya msukumo wakati moyo unadunda kusukuma damu.
Shinikizo au presha ya diastole ni kipimo
cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa wakati moyo
umepumzika au kati ya mapigo ya moyo.
Kinachosababisha shinikizo la damu
NIMR inaeleza kwenye taarifa yake kuwa
kinachosababisha shinikizo la damu (hakijulikani katika asilimia 90% ya watu
wenye tatizo hilo lakini ) unene wa kupindukia (Vitambi), matumizi ya chumvi nyingi
kwenye chakula, kutoshughulisha mwili kwa mazoezi au kazi zinazotoa jasho,
uvutaji wa sigara na unywaji pombe wa kupindukia.
Mambo mengine yanayoweza kusababisha ni mazingira
ya mfadhaiko, msongo wa mawazo ama sonona, ulaji wa vyakula vingi vya wanga,
sukari na mafuta na wakati mwingine historia ya familia kusumbuliwa na tatizo
hilo. Hii ina maana tatizo linaweza kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi
kingine.
Jinsi ya kujikinga
Kuna mambo mengi ambayo mtu anaweza kufanya
ili kuzuia kupata shinikizo la damu. Miongoni ni kuacha matumizi ya tumbaku,
kuwa na uzito unaowiana na urefu, fanya mazoezi ili kuimarisha hali ya afya ya
moyo angalau mara tatu kwa dakika 30 kila wiki.
Mambo mengine ni kupunguza matumizi ya
chumvi nyingi kwenye vyakula, punguza unywaji wa pombe na pia punguza ulaji wa
vyakula vyenye wanga mwingi na ikiwezekana nafaka zisizokobolewa.
Mtu anapaswa pia kupunguza ya vyakula vyenye
mafuta mengi kupunguza uwezekano wa mwili kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu
ama kama ilivyozoeleka kwa jina la kolestero.
Kwa watu wazima umri zaidi ya miaka 18
inabidi kupima shinikizo la damu mara kwa mara na kula vyakula vyenye vitamin
kwa wingi kama vile matunda na mboga za majani.
Dalili za Shinikizo la Damu.
Kuumwa kichwa, uchovu, matatizo ya macho,
kichefuchefu, kutapika, Hali ya woga, Hali ya kuchaganyikiwa, kupauka kwa ngozi
au kuongezeka wekundu wa ngozi.
Dalili nyingine ni kukosa usingizi, kuhisi
kizunguzungu, kuwa na hamu ya chumvi, kitambi, hasira mara kwa mara, kuwa na
hali yakufanya vitu haraka na kukosa uvumilivu, kiharusi na kutokwa jasho sana.
Kudhibiti
shinikizo la damu
Kula vyakula vyenye afya, punguza vyakula
vyenye chumvi, mafuta, kolestero na wanga. Dhibiti mifadhaiko, kupunguza
mifadhaiko au kutafuta njia ya kudhibiti mifadhaiko.
Fanya mazoezi; dakika thelathini ikiwezekana
dakika 30 kila siku, kuwa na uzito sahihi kulingana na urefu na pata ushauri wa
daktari au kuhudhuria kliniki unapobainika unaugua shinikizo la damu.
Kutodhibiti shinikizo la damu ni rahisi
kupata kiharusi, tatizo la kuona vizuri, kuharibika kwa mishipa ya damu na
ubongo, moyo kushindwa kufanya kazi na matatizo ya figo.
Taarifa hii imeandaliwa na Jukwaa la
Waandishi wa Habari Wanaopambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TJNCDF), SLP
13695, Dar es Salaam. Baruapepe: tjncdf@yahoo.com
Simu: +255 713 247 889
SHARE
No comments:
Post a Comment