JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
KUHUSU UPOTOSHWAJI WA TAARIFA ZILIZOANDIKWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KIJITOUPELE
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inapenda kutaarifu Umma na Watanzania kwa
ujumla kuwa Jimbo la Kijitoupele lililoko Zanzibar ni miongoni mwa
Majimbo hamsini(50) ambayo yalitegemewa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25,
oktoba,2015.
Hata
hivyo Jimbo hilo halikufanya uchaguzi wake wa Mbunge kutokana na
hitilafu katika karatasi za kupigia kura badala Wapiga kura walishiriki
katika kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Tume
imefikia uamuzi wa kutoa ufafanuzi huu kutokana na taarifa
iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi toleo l Na.322 la Januari 18,
2016 katika ukurasa wake wa mbele likidai “ NEC YAIBUA MAPYA” Habari
hii si sahihi na inalenga kuupotosha umma na kuleta uchochezi miongoni
mwa Wananchi.
Kwa
ujumla maelezo yote yaliyopo katika taarifa hiyo yanaeleza kwamba, Tume
imeanzisha Jimbio jipya, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti husika ni
Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inapenda inasisitiza kuwa taarifa zilizotolewa na
Gazeti la MwanaHALISI siyo za kweli, ni za uongo, uzushi, uzandiki na
uchochezi. Kufuatia taarifa hiyo,Tume inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
• Tarehe
13 Julai, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Vyombo vya
Habari ikionesha Orodha ya Majimbo yatakayofanya uchaguzi wa Mkuu wa
tarehe 25 Oktoba, 2015 na Jimbo la Kijitoupele lipo katika Orodha hiyo.
Taarifa hii ipo katika tovuti ya Tume.
• Katika
Taarifa hiyo, Tume ilieleza wazi kuwa Majimbo ya Zanzibar yataendelea
kuwa hamsini (50), ingawaje Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeongeza
majimbo manne na kuwa Hamsini na Nne (54).
• Tulieza
sababu ya kubaki na Majimbo hamsini (50) ni kutokana na matakwa ya
Ibara ya 98 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 ambayo ili kuongeza idadi ya wabunge kutoka Zanzibar
inahitaji theluthi mbili ya Wabunge kutoka Tanzania Bara na theluthi
mbili ya Wabunge kutoka Zanzibar kuunga mkono mabadiliko hayo.
• Tulieza
kuwa, kipindi hicho Tume isingeweza kuandaa na kuwasilisha Muswada
Bungeni kwa kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa
linamaliza muda.
SHARE
No comments:
Post a Comment