TRA

TRA

Tuesday, January 19, 2016

Uzinduzi wa Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana Zanzibar Young Pioneers.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 
Maveterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Maveterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakipiga makofi wakati wa kuingia mgeni rasmin Mhe Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee kwa ajili ya uzinduzi wa Jumuiya hiyo kuendeleza Vijana Zanzibar.
Ustadh akisoma Quran kabla ya Uzinduzi huo wa Jumuiya ya Veterani wa Umoha wa Vijana wa Young Pioneers uliofanyika katika ukumbi wa ZSSF kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Maveterani wa Young Poineers wa Umoja wa Vijna wakimsikiliza msoma quran wakati wa uzinduzi huo.
Katibu wa Veterani wa Young Pioneers Said Shaban akitowa maelezo ya Jumuiya hiyo ya Veterani wa Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wake uliofanyika katika Ukumbi ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. 
 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Veterani wa Young Pioneers, Mhe. Khadija Hassan Aboud akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mhe Asha Ali Abdalla akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya ya Veterani ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers, katika Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia Veterani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa ZSSFKiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. na kutangaza Fedha zilizopatika katika harambee aliyoiazisha kwa ajili ya kukuza Mfuko wa Jumuiya hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 9,724,000/= zimepatika ikiwa Fedha Taslimu Shs 3.874,500 na Ahadi Shs.5,850,000/=

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger