Katibu wa
wilaya ya Same Mhe. Evagry Keiya (katikati) akikata utepe kufungua duka
la Tigo Same, wanaoshuhudia ni Meneja wa huduma kwa wateja Tigo,
Mwangaza Matotola(kushoto) na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini
George Lugata(kulia) mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tigo wakiwa katika tafrija ya ufunguzi wa duka la Tigo Same mapema wa mwishoni wa wiki iliyopita.
Mkurungezi
wa Tigo kanda ya kaskazini Bw.George Lugata akitoa hotuba wakati wa
ufunguzi wa duka la Tigo Same mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Baadhi ya
wageni waalikwa wakiwa kwenye tafrija ya kufungua duka la Tigo same
wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mh Evagry Keiya mapema
mwishoni wa wiki iliyopita.
Kampuni
ya simu ya Tigo imefungua duka jipya la same ambalo limepunguza adha
kwa wateja wa kampuni hii ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa wateja
umbali mrefu toka kwa makazi yao
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo Kanda ya kaskazini
Bw.George Lugata alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya mipango ya
kampuni ya Tigo kusogeza huduma karibu na wateja wake.
“Kampuni
ya tigo imeangalia fursa zilizopo katika eneo la Same ambapo kwa pamoja
tumeiona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana na wakulima na wafanya
biashara kuweza kufanya huduma mabalimbali za kibenki kwa kutumia simu
za mkononi”Alisema Lugata
Aliongeza kuwa ufunguzi huo unaendana na kuboresha muonekano wa duka hili kuwa wa kisasa
Lugata
alisema kuwa duka hilo linalopatikana katika mtaa wa shule linategemea
kuhudumia wateja wapatao mia tatu kwa siku wakipata huduma mbalimbali
ikiwemo huduma za kuunganishwa kwenye intaneti, usajili wa laini za simu
na kurudisha laini zilizopotea pia kununua simu za kisasa.
Kwa
upande wa Katibu wa Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe. Evagry Keiya alipongeza
hatua za Tigo za ufunguzi wa duka hili kwa kuwa utarahisisha
upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wilaya ya same.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment