Agizo hilo lilitolewa Dar es Salaam hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Alphaya Kidato wakati akizungumza katika mahafali ya nane ya Chuo cha Usimamizi wa Kodi.
“Kuanzia sasa hadi Juni tutajikita katika maeneo yote ambayo watu hawalipi kodi," alisema.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa fedha zitakazopatikana zitasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuboresha huduma za kijamii.
Alisema kwa kipindi kirefu wamelaumiwa kwa kutokusanya kodi, hivyo kwa sasa mamlaka inaelekeza nguvu zake katika eneo hilo ili kila anayetakiwa kulipa kodi alipe.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mahafali hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema Serikali haiwezi kuendelea bila watu kulipa kodi.
Alisema vijana waliohitimu watasaidia kuelekeza jamii kuhusu umuhimu wa kulipa kwani dhamira ya Serikali ni kuendelea kukusanya mapato na si kwa Desemba.
"Utawala wetu wa ukusanyaji wa mapato unasema huu mwaka ni mwanzo kwani nia tunayo na wataalamu wameongezeka, hivyo tutatimiza malengo yetu," alisema Kijaji.
Mkuu Chuo cha Kodi, Profesa Isaya Jairo alisema wana mafanikio kwa mwaka huu kwani wamepata wahitimu 538 waliongezeka kwa kiasi kikubwa na wamepitia upya mitaala na kuongeza daraja la walimu.
Hata hivyo, alisema wana mpango wa kuanzisha kampasi mpya Kibaha (Misugusugu) kwa ajili ya kuendelea kuongeza idadi ya wanafunzi.
SHARE
No comments:
Post a Comment