Wasichana walitekwa kutoka shule ya Chibok. Jeshi la Nigeria linasema limemwokoa msichana mwingine wa pili
Jeshi la
Nigeria limesema kuwa msichana mwingine aliyetekwa na wanamgambo wa Boko
Haram zaidi ya miaka miwili iliyopita kutoka shule ya Chibok
ameokolewa.
Msemaji
wa Jeshi kanal S K Usman hakueleza kwa undani namna ambayo msichana huyo
ambayr hakutajwa jina aliokolewa,lakini akasema patakuwa na maelezo
zaidi baadae.
Siku ya
Alhamisi msichana mwingine mwenye miaka 19 ambaye alifnikiwa kutoroka
katika kambi ya Boko Haram, Amina Ali Nkeki,alipelekwa katika mji mkuu
Abuja akiwa na mtoto wake alizaliwa wakati ametekwa, kwa ajili ya
kukutana na Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari.
Zaidi ya
wasichana wengine mia mbili bado hawajapatikana,huku ikidhaniwa kuwa
bado wanashikiliwa katika misitu ya Sambisa karibia na mpaka wa
Cameroon.Gavana wa jimbo la Borno amesema kwamba jeshi la nchi hiyo
limejiandaa kuwakomboa wasichana hao.BBC
SHARE








No comments:
Post a Comment