Kipindi
hiki cha utawala wa awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John
Magufuli, unapotaka kuzungumzia muziki wa Bongo Flava ni vigumu
kuepuka kutaja la Diamond Platnumz na Alikiba.
Muziki
wao, ushindani na maneno ya hapa na pale yanatoa picha halisi ya game
ya muziki huo ilivyo kwa sasa. Kutokana na uzito wa majina yao na kile
kinachoripotiwa kuwa hawapatani (beef) si ajabau kusiki watu maarufu
wakiwazungumzia. Makala haya fupi yanakuletea watu maarufu waliozungumza chochote kuhusu wawili hawa.
Amani
Msanii huyo kutoka nchini Kenya katika mahojiano yake na kituo cha
Radio Citizen March 2016, alizungumzia jinsi Diamond na Alikiba
anavyolipwa fedha nyingi pindi wanapoenda kufanya show katika nchi hiyo
kitu ambacho alisema si kibaya.
Ni
kitu ambacho kipo kila mahali, hata ukienda kuperform Rwanda atakuta
wewe unalipwa hela nyingi zaidi vile wanalipwa, lakini pia wasanii
wajitahidi ili waweze kushindana katika jukwa la Afrika Mashariki na
Afrika at least wawe na kitu kinaitwa bargain power.
Nyimbo
zako zikiwa ni hit zina video ambazo ni kali uko na bargain power na
unaweza itisha kiasi cha juu zaidi kwa hiyo ni hali ya biashara hamna
haja ya kuumia.
Kuna
watu ambao sio lazima wawe na hit lakini huyo mtu akishika hiyo stage
anaperform quality show na utakuta hao watu huperform kwenye hizi event
za mabalozi hulipwa fedha nyingi sana.
2. Ruge Mutahaba
Ni
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, November 2016
kupitia XXL alizungumzia team ambazo kazi yake ni kuwashabikia Diamond
na Alikiba na kueleza namna wasanii hawa wanavyoweza kunufaika kwenye
hilo na mathara yake.
Ishu
ya team zilikuwepo na haziitakaa kuacha kuwepo, tatizo la team ni
kwenye athari za wale wanateam, yaani mimi naamini team ni muhimu kwa
sababu zinaleta ushindani lakini team ya kumshangilia kwenye mitandao
kwangu sioni kama ni team ya ukweli.
Team
ni kusapoti mpaka mwisho, team ni akifanya tamasha wale wa team nusu
yao wamo ndani, ndio tuzungumze team kwa maana hiyo na hizo ndizo
zilikuwa team Simba, Yanga, Liverpool, Manchester, team inamnunua
mchezaji inarudisha hela siku hiyo hiyo kwa jezi kununuliwa na watu wale
wa ndani ya hiyo team.
Lakini
hii team ya kushabiki juu kwa juu kweli kwangu haina athari sana kama
haitaleta athari ya kibiashara inabakia ni ushabiki tu wa kawaida.
Inaweza
kuleta matatizo, matatizo ya Tupac na B.I.G sikulikuwa na team, Tupac
alipigwa siasi na watu wa B.I.G, tuombe Mungu yasitokee matitzo hayo.
Kwa bahati mbaya huwezi kulazimisha kwa kutokuwepo kwa team kwa sababu
wapo wanaopenda Msondo na wanaopenda Sikinde, suala ni kwamba
unasaidiaje kile unachokipenda kiwe na maana na kizidi kukua.
3. Salim Kikeke
Mtangazaji
huyo wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, September 2015 katika kipindi cha
Mkasi kilichokuwa kikiruka EATV aliulizwa kati ya Alikba na Diamond
anafikiri nani mbabe zaidi.
Nisingependa
kuchukua upande mimi naheshimu kazi zao na wote nimefanya nao kazi,
Alikiba sijawahi kufanya nae interview lakini nakumbuka tulishapanga
tukakubaliana kabisa tufanye lakini akapata safari. Diamond alipokuja
Uingereza nikamwanbia ukiwa na nafasi njoo kwenye kipindi chetu
akakubali na akaja tukafanya nae interview.Kwa mtazamo wangu mimi kama
mwandishi wa habari ambaye pia napenda kukuza muziki wetu wa Tanzania
nasema sichukui upande wowote naheshimu kazi zao.
4. Vera Sidika
Huyo
ni video vixen kutoka nchini Kenya, August 2016 katika mahojiano na
Bongo5 aliulizwa kati ya Diamond na Alikiba anamkubali nani zaidi.
Mimi
namsikiliza Diamond, muziki wake na stayle yake ni tofauti kisha nzuri
pia namuona anarelease hit after hit, hatulii yeye hutia bidii kila siku
halafu si muziki pekee yake pia anaweza kusaidia vijana na kuwapatia
nafasi ya kukuza vipaji vyao kama sasa hivi kuna artists wapo chini yake
which is good thing.
Mtu
ukiwa katika industry especially music it good to empower the people
maana yake kuna watu wengi wanakuangalia wewe na wana kipaji lakini
hawajui waende vipi sasa wewe ukiwaonyesha direction inakuwa ni vizuri
sana.
5. Dkt. Harrison Mwakyembe
Kwa
sasa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, March mwaka huu
baada ya kupata taarifa ya kuwa Diamond na Alikiba wameshindwa kurekodi
wimbo kwa ajili kuhamasisha watu kuichangia timu ya taifa ya vijana
chini ya miaka 17, Serengeti Boys alisema atahakikisha wanapatana.
Hao
vijana niwaite hapa Dodoma na sitaki kusikia wengine wanasema unajua
wale hawakai pamoja, hamna lolote mimi baba yao watakaa pamoja, hapa
tupo kwenye mambo ya taifa, hili ni suala la kitaifa lazima
tulifanikishe na kila mtu achangie.
6. Dudu Baya
Msanii
huyo wa Bongo Flava July 2014 kupitia Amlifaya ya Clouds Fm aliwataka
Diamond na Alikiba kutambua wao ni wakina nani na wana uwezo wa kufanya
nini, pia watumie fan base walionayo kujinufaisha kibiashara kuliko
kusikiliza maneno ya watu ambayo yamelenga kubomoa.
Alikiba
alifanya ngoma na R Kelly mimi nilifurahia sana nilipenda kinoma na
nikapiga saluti kwa kuwa mdogo wangu kwamba anaenda next level, Diamond
kaja kufanya vizuri nina appreciate.
Muziki
unakosa power kwa sababu ya watu kuwa na roho mbaya na chuki na
kutokuwa makini na watu waliotuzunguka, kuna mtu anaenda kwa Alikiba
anasema hivi, anaenda kwa Diamond anasema hivi.
Kwa
hiyo hawa kama wadogo zangu mimi nawashauri watulie chini wajitambue
wao ni wasanii na usanii wao ni wa kutengeneza pesa, tena hata
watengeneze tour ya amani wazunguke nchi nzima watengeneze hela na si
beef.
7. Kingwendu
Mchekeshaji
huyo January 2016 aliiambia Bongo5 kuwa yeye akipata airtime katika
radio na tv kama wanavyopata diamond na Alikiba atafika mbali kimuziki.
Mwaka
jana nimetoa nyimbo tatu lakini zote hazikupata airtime ndio maana
hazikufanya vizuri lakini kwa sababu ni nyimbo nzuri zingepata airtime
ningeshindana na akina Ali Kiba na Diamond ambao wanafanya vizuri.
Sijakata
kataa, mwaka huu kuna kazi mpya nimeziandaa pamoja na video mpya. Pia
nikifanikiwa kupata meneja wa kusimamia muziki wangu natumaini nitafika
mbali sana kwa sababu muziki wa sasa ni mipango tofauti na ule wakati
nimetoa Mapepe.
Nimejaribu
kugusa kila kona ambayo kwa namna moja au nyingine inahusika katika
muziki wa Bongo Flava ili kujionea nguvu ya ushawishi walionayo Diamond
na Alikiba. Kufikia hapa sina budi kuweka kalamu yangu chini, asante
sana.
SHARE
No comments:
Post a Comment