TRA

TRA

Friday, May 6, 2016

WAFANYAKAZI WA NHC WAPANDA MITI KATIKA MAKAZI YALIYOUZWA KWA WANANCHI KIBADA NHC

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susani Omari akizungumza na Mameneja wa NHC na Wakurugenzi wakati wa zoezi la kupanda miti katika Estate ya Kibada ikiwa ni jitihada za NHC kuboresha mazingira ya eneo hilo linalokaliwa na wakazi takribani 1,000 katika nyumba zipatazo 218 za gharama nafuu. EMT wote(Directors, Regional Managers &  Line Managers) pia wametembelea miradi ya Kawe, Morocco Square, Victoria Place, Eco Residence na Kibada ambako kumefanyika shughuli hiyo ya upandaji miti.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akipanda mti wa mchikichi katika eneo la makazi la NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TAMICO), Lilian Reuben na Meneja wa NHC, Mtwara, Joseph John wakipanda mti katika eneo la makazi la NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate.
Zoezi la kupanda miti likiendelea katika eneo la makazi la NHC Kibada Kigamboni maarufu kama Kigamboni Housing Estate.(P.T)
Read more...

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI

Published in Jamii
Z1
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed ambae alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr, (kulia) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu  Wizara hiyo Halima Maulid Salum.
Z2
Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr akisoma risala ya wakunga katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Z3
Mwakilishi wa Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) akitoa salamu za Shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Z4
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger