Bunge
limepitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya serikali yenye malengo ya
kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi Triln 29.54, ambapo asilimia 40
ya fedha hizo zitatumika kwaajili ya miradi ya maendeleo na kiasi
kilichobaki kitatumika kwa matumizi ya kawaida.
Idadi
ya wabunge walioshiriki kupiga kura walikuwa 251 na wote wamepiga kura
za ndiyo na kuipitisha bajeti Kuu hiyo kwa asilimia 100 pamoja na
kupitisha sheria ya fedha kwa mwaka 2016/2017.
Picha
zote zinahusu matukio yaliyotokea ndani na nje ya viunga vya Bunge mjini
Dodoma, ikiwemo wabunge na baadhi ya wananchi waliohudhuria
uhitimishaji wa Bajeti hiyo, wakimpongeza Waziri na watendaji wa Wizara
ya Fedha na Mipango kwa kufanikisha kazi kubwa ya kuandaa bajeti hiyo.
Picha zote na WFM
Imetolewa na
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
SHARE








No comments:
Post a Comment