Mamia
ya vijana walijitokeza katika usaili wa mashindano ya Maisha Plus
mwishoni mwa wiki ili kufanya usaili wa mashindano hayo kwa msimu wa
tano.
Mashindano
hayo yalifanyika katika kijiji cha Makumbusho Kijitonyama jijini Dar es
salaam ambapo vijana waliojitokeza waliulizwa maswali mbalimbali
ikiwemo mtazamo wao juu ya mwenendo wa kiuchumi ndani na nje ya
Tanzania, afya, kilimo, ufugaji na mengine.
Vijana waliofanyiwa usaili walitoka mkoa wa Dar es salaam pamoja na mikoa ya jirani ikiwemo Pwani.
"Maswali
yetu huwa hayana utaratibu, wala sio maswali ambayo mshiriki anaweza
kujiandaa. Mengi huwa yanakusudia kupima uelewa wa mshiriki juu ya
maswala mbalimbali ya kidunia na namna anavyoweza kukabiliana na
changamoto mbalimbali." Alisema Masoud Kipanya, Jaji na mwanzilishi wa
mashindano ya Maisha Plus.
Akitaja
vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na
waanzilishi wa Maisha Plus alisema, "Tunachukua washiriki wenye umri wa
miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia
kutoka nchi za Afrika Mashariki"
Maisha
Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi
tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo
mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya
kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni
'Vijana Ndio Ngazi'.
Usaili
unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania.
Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio
mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali
ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo ya www.maishaplus.tv
SHARE








No comments:
Post a Comment