Mwenyekiti
wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimkabidhi kadi ya uanachama
Goodluck Ole Medeye aliyekuwa mwanachama wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA jana kwenye Makao Makuu ya Chama hicho Mwananyamala
Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimshuhudia Bw. Goodluck Ole
Medeye wakati akionyesha kadi ya uanachama aliyokabidhiwa baada ya
kujiunga na Chama cha UDP akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA jana kwenye Makao Makuu ya Chama hicho Mwananyamala Kinondoni
jijini Dar es salaam.
wenyekiti
wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimpongeza mke wa Goodluck
Joseph Ole Medeye mara baada ya mume wake kujiunga na Chama cha UDP
jana.
Kada wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, aliyedumu na chama hicho kwa
miezi kumi na moja Goodluck Ole Medeye, amekihama chama hicho na
kujiunga na United Democratic Party UDP.
Bw.
Medeye aliyewahi kuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na
kuitumikia serikali katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, ametangaza uamuzi wa kuhama Chadema jijini Dar es
Salaam na kukabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa Chama hicho John
Momose Cheyo.
Mbunge
huyo wa zamani wa jimbo la Arumeru Magharibi amejiunga na UDP akiwa na
Mkewe, pamoja na watu wengine tisa wakiwemo waliokuwa kwenye vyama
tofauti na wengine waliodai hawakuwahi kuwa kwenye siasa, ambapo katika
maelezo yake, Ole Medeye amesema awali alitaka kuunda chama kipya lakini
baada ya kupitia katiba za vyama akaona UDP ni sehemu sahihi.
Kuhusu
masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, wanasiasa hao wamelaani
uminywaji wa demokrasia katika kipindi hiki, hususan ndani ya Bunge, na
kushauri wabunge wa kambi ya upinzani wanaosusia vikao kurejea ndani ya
ukumbi wa Bunge kwa vile njia wanayotumia haitabadili utaratibu wa
kibunge hususan kumuondoa Naibu Spika kwenye kiti chake.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment