Watu 50
sasa wanajulikana kuuawa kwa kupigwa risasi wakati wa shambulizi
lililotokea kwenye baa moja katika jimbo la Florida, na kuwa moja ya
mashambulizi mabaya zaidi katika historia ya Marekani.
Watu
wengine 50 wako hospitalini. Vyombo vya habari vimemtambua mwanamme
ambaye alitekeleza shambulizi hilo katika mji wa Orlando kuwa raia wa
Marekani, Omar Mateen.
Omar Mateen, aliyefyatua risasi Orlando
Mwanamme
huyo wa umiri wa miaka 29, alikuwa amejihami kwa bunduki mbili wakati
alifyatua risasi katika baa ya Pulse siku ya Jumaosi
Aliwashika mateka karibu watu 30 kabla ya polisi kumpiga risasi na kumuua.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment