Balozi
wa Huawei Brenda Muchunguzi(Kushoto) akimuonyesha mteja wa Huawei Bw.
Wilson Tendwa(Kulia) ubora wa simu mpya ya GR5 katika duka la Huawei
lililopo J Mall Dar es Salaam.
Balozi
wa Huawei Brenda Muchunguzi(Kushoto) akimuonyesha mteja wa Huawei Bw.
Wilson Tendwa(Kulia) ubora wa camera ya simu mpya iliyozinduliwa ya GR5
katika duka la Huawei lililopo J Mall Dar es Salaam.
Balozi
wa Huawei Jamila Feruz (Kulia) akimuonyesha mteja wa Huawei Bw. Jacob
Kaiza (Kushoto) ubora wa simu mpya iliyozinduliwa ya GR3 katika duka la
Huawei lililopo City Mall Dar es Salaam.
Huawei kukidhi mahitaji ya kizazi kipya na simu zenye gharama nafuu.
Dar es
Salaam, Juni 2016: Baada ya mafanikio katika uzinduzi wa simu inayodumu
na chaji kwa zaidi ya masaa 90 ya Y6 Pro nchini Tanzania hivi
karibuni; Huawei, kinara wa uvumbuzi ulimwenguni katika mawasiliano na
teknolojia, wamezindua simu mbili za bei nafuu, Huawei GR 3 na GR 5
katika soko la Tanzania mwezi huu. Miongoni mwa bidhaa zingine, simu
hizi zinalenga vijana na watu mbalimbali nchini Tanzania ambao wanakuwa
na shughuli nyingi kwa siku.
Vijana
ndio waliohamasisha muundo wa simu ya GR 3 Na GR 5. Simu hizi mbili
zimeundwa mahususi kwa ajili yao. Na haijalishi una umri gani ila kama
una ashiki ya ujana basi we ni kijana; Muundo wa simu hizo mbili
unazifanya kuvutia Zaidi hii ni kutokana na kifaa chenye Uwezo wa
kutambua alama za vidole za mtumiaji kwenye GR 5 na kamera ya MP 13
kwenye GR 3. GR 5 ni simu rahisi kutumia, ikiwa na muundo wakumsaidia
mtumiaji awe na matumizi rahisi.
Akiongea
kuhusiana na simu hizo mpya, Mkurugenzi wa mauzo ya rejareja wa Huawei
Tanzania Bwana Slyvester Manyara alisema Huawei GR 3 na GR 5
zimetengenezwa ili kuendana na vijana katika shughuli zao za kila siku
kuanzia muundo wake mpaka matumizi. “Huawei inafikiria daima namna mpya
za kuboresha huduma kwa wateja wetu na tunafuraha kuwa tunafanikisha
jambo hili” alisema Bwana Manyara.
Akiongelea
mabadiliko ya matumizi ya simu za mkononi nchini Tanzania Bwana Manyara
alisema mwanzoni simu hizi za kisasa zilitengenezwa kwa ajili ya watu
wenye fedha na kazi za kipato kikubwa ambao wangeweza kumudu bei, kwa
ujumla Huawei imejitahidi kuwepo na simu za smartphone kwa kila daraja
la wateja bila kujali kipato chao. Tukiwa na lengo la kufikia watu wa
soko la chini hadi la kati, tumeamua kuzindua GR5 na GR3. Simu hizi
zimetengenezwa kukidhi mahitaji tofauti ya wateja wetu tukiangalia zaidi
kipato chao. GR3 na GR5 ni simu za bei nzuri pia zina vitu mbalimbali
vya kuvutia kwa ajili ya watu walio katika maisha ya kawaida na kazi za
kuwafanya wazunguke au kutembea sana.
“Kwa
sasa kuna ongezeko kubwa la mawasiliano ya kijamii nchini Tanzania kama
Twitter, Whatsapp, Instagram na Facebook. Watanzania wengi wanapenda
unafuu, wepesi na urahisi katika mitandao hii kwa ajili ya mawasiliano
yao kila siku. Simu za Huawei zimeundwa vyema na zina fanya kazi kwa
ufasaha na zinapatikana kwa bei rahisi. Simu mpya za kuvutia za Huawei
katika mlolongo wake wa G zinarudisha thamani ya fedha yako”, alikazia
Mkurugenzi wa Mauzo ya Rejareja.
Kwa
mujibu wa Meneja wa Huawei nchini Tanzania, Bwana Huxiangyang Jacko, GR5
ina teknolojia mpya ya Uwezo wa kutambua alama za vidole ambayo
huifanya iwe haraka na yenye usalama zaidi ukilinganisha na matoleo ya
awali.
“Uwezo
mkubwa wa kutambua alama za vidole za mtumiaji wa simu uliopo katika
GR5 unaleta uwezo mkubwa ambao unaongeza matumizi mepesi na uelewa mzuri
kwa mahitaji ya mtumiaji. Toleo hili la pili la Uwezo wa kutambua alama
za vidole linapelekea ufanyaji kazi wa haraka Zaidi na mwepesi kuliko
toleo la kwanza uliokuwepo katika simu za awali. Inasaidia pia kwenye
kuangalia na kufuta vitu kwa haraka na kupiga picha au kupokea simu
haraka” , alisema Bwana Jacko.
Ikiwa
na vitu mbalimbali na muundo wa kuvutia simu hizi zina vifaa
vilivyoundwa mahususi kwa kumuunganisha kijana wa Kitanzania na simu
sahihi. Kwa mujibu wa Huawei Tanzania, simu hizo mbili zina 4G. Pia zina
LTE ili watumiaji waweze pakua vitu kiurahisi Zaidi, kuangalia filamu
na simu ina nafasi ya kuhifadhi vitu GB 16.
GR3 na
GR5 zisingekua simu za Huawei bila kuwa na kamera zenye ubora wa juu.
Kamera zinauwezo wa kupiga picha kwenye mwanga hafifu na kutoa picha za
viwango vya juu. Huawei GR3 Na Gr5 inawapa watumiaji uwezo kuiona dunia
kwa uwezo mkubwa zaidi.
Kwa
maneno ya Chades Charles Lwamlema, kijana wa kitanzania anayefanya kazi
katika moja ya mashirika ya kiserikali nchini, amesifia Huawei Tanzania
kwa hatua kubwa waliopiga kufikia kizazi cha sasa kwa simu za kisasa za
bei rahisi, simu ambayo imemsaidia katika kazi yake na maisha yake kwa
ujumla.
Ushuhuda wa uwezo mzuri wa Huawei GR3 na GR5 unaendeleza nia ya dhati ya Huawei kuwa na simu zenye ubora mkubwa katika soko.
Kuhusu Huawei.
Huawei
huongoza duniani katika Teknologia ya Mawasiliano. Ikibuni wakati wote
kwa kuzingatia mahitaji ya wateja, wamejikita katika kuongeza uzoefu wa
wateja na kuleta thamani ya juu kwa mashirika ya simu, makampuni na
wateja. Vifaa vya mawasiliano ya simu ya Huawei, bidhaa za Teknologia ya
Mawasiliano, na simu za kisasa hutumika katika nchi 170 ulimwenguni.
Huawei
ipo nafasi ya 3 katika usambazaji wa simu (2015) ilikiwa imesambaza
zaidi ya simu milioni 110 ulimwenguni. Huawei Tanzania imedhamiria kuwa
kinara katika bidhaa borana za kisasa ulimwenguni, ikiwa inatoa huduma
za simu internet rahisi zaidi kutumiwa na wateja. Kwa sasa, Huawei
Tanzania ipo nafasi ya 2 ikiwa na hisa za soko la 22% (katika robo ya
kwanza ya mwaka 2016)
SHARE








No comments:
Post a Comment