RUFAA YA MAMA NA MTOTO KUTOLEWA KWA HUDUMA YA SIMU.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKUU
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amesema kuwa mfumo wa mawasiliano wa
kuboresha huduma ya Rufaa ya mama na mtoto kutasaidia akina mama na
watoto wachanga huduma bora na matibabu wanayohitaji katika hospitali za
rufaa.
Mushi
ameyasema hayo leo wakati Uzinduzi wa mfumo wa mawasiliano wa
kuboresha huduma ya Rufaa ya mama na mtoto , amesema kufanya
mawasiliano ni njia ambayo inafanya mgonjwa kupata huduma bora.
Amesema
kuwa huduma hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam, imefika kwa muda mwafaka
kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu hivyo hata huduma zinatakiwa
kuboreshwa.
Aidha
amesema kuwa matumizi ya simu kwa vituo vya afya 127 vitaleta matokeo
chanya na kuwa chachu kwa vituo vitakavyofuata kuendesha huduma hiyo
itaweza ku huduma ya mama na mtoto.
Naye
Meneja Mradi wa CCBRT, Brenda D’mello amesema kuwa Kamati ya Afya ya
Mkoa wa Dar es Salaam , ikishiriakiana na CCBRT wanapambana na tatizo
hafifu kati ya zahanati vituo vya afya na Hospitali.
Amesema kuwa na mawasiliano hafifu husababisha rufaa ya wagonjwa usio na mpangilio na ucheleweshwaji wa huduma na matibabu.
Brenda
amesemavituo 23 na magari ya wagonjwa saba (7) yataunganishwa na mfumo
wa simu pamoja na ofisi za waganga wakuu wa wilaya na matabibu wa wa
timu ya afya ya mkoa.
Muuguzi akitoa mfano wa utoaji wa huduma kwa mama kwajia ya mfumo wa mawasiliano.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda katika uzinduzi wa Mpango wa mfumo wa mawasiliano
kuboresha huduma za Rufaa kwa mama na mtoto. Akitoa simu Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Mwananyamala, Aziz Msuya simu hiyo kwaajili ya kuboresha
huduma hiyo.
Watendaji waliokabidhiwa simu maalum za mawasiliano kwaajili ya kutoa huduma za dhalula kwa mama na mtoto.
SHARE








No comments:
Post a Comment