Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw.
James Mlowe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano
huo.
HASSAN SILAYO
Mfuko wa
Pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama wapya 27, 362 katika
mwaka wa fedha wa 2014/2015 tofauti na mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo
walisajili wanachama 23,228.
Hayo
yamesemwa na Meneja wa Elimu na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw.
James Mlowe wakati na mkutano wa waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.
Bw. Mlowe
alisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na huduma na mafao bora yenye
wigo mpana na kugusa moja kwa moja maisha ya mtanzania ambapo wamepanga
kufikia wanachama 180,000 kufikia mwezi June 2016.
Mlowe
aliongeza kuwa miongoni mwa sekta zilizoingiza wanachama wapya kwa mwaka
2014/2015 ni Walimu ambapo imetoa wanachama 39,537, Zimamoto na
uokoaji wanachama 851, Polisi na Uhamiaji wanachama 415 na Magereza
wanachama 205.
Aidha Bw.
Mlowe aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 mfuko huo
ulikusanya kiasi cha shilingi bilioni 210.069 ikiwa ni ongezeko la
asilimia 31.9, ambapo wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 286
billioni kufikia mwezi Juni 2016.
Pia Mfuko
huo umesajili waajiri wapya 88 katika kipindi cha mwaka 2014/2015 na
unategemea kuendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na mfuko huo
kuendelea kuboresha huduma zake.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment