Rais Paul
Kagame anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam, nchini
Tanzania Julai 1 kwa mwaliko wa mwenzake wa Tanzania Rais John Pombe
Magufuli.
Katika
ziara hiyo Rais Paul Kagame atafungua mkutano wa kimataifa wa 40 wa
wafanyabiashara, Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) na
kufanya mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano baina ya nchi
hizi mbili.
Kwa
mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,
Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, rais wa
Rwanda atafanya ziara ya kikazi nchini Tanzania baada ya kualikwa na
mwenziye wa Tanzania, Rais John Magufuli.
Wakati wa
ziara hiyo, Bw Kagame na ujumbe wake wanatarajiwa kutia saini Mkataba
wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili (MoU), ambo ulikamilishwa na
kamati ya pamoja ya wataalam kutoka nchi zote mbili.
Nchi hizi
mbili jirani, mwezi uliopita, zilikubaliana kuunda kamati ya pamoja ya
utekelezaji (JIC) itakayofuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi
muhimu, wakati wa kikao cha 14 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC).
Kamati
hii ilikubaliana kuimarisha mahusiano baina ya nchi katika sekta
mbalimbali muhimu, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano katika sekta
ya usafiri wa anga, hasa kati ya mashirika ya ndege ya nchi hizi mbili,
Rwandair na Air Tanzania.
Katika
mkutano huo pia walikubaliana kuboresha miradi ya maendeleo, ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa barabara itakayounganisha nchi tatu ambazo ni
Burundi, Uganda, na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) .
Mambo
mengine ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili ni pamoja na kuongeza
kasi kwa ujenzi wa reli utakaogharimu matrilioni ya Shilingi za
Tanzania.
Itafahamika
kwamba Rais Paul Kagame atakua rais wa pili kutembelea Tanzania, toka
Rais John Pombe Magufuli achukuwe hatamu ya uongozi wa nchi, baada ya
Rais wa Viet Nam, Truong Tan Sang.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment