TRA

TRA

Tuesday, June 28, 2016

TAARIFA YA UTEUZI KWA VYOMBO VYA HABARI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


index
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye amemteua Dkt. Herbert F. Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Uteuzi huu umefanywa chini ya Kifungu Na. 9 (1) cha Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambacho kinampa Waziri mamlaka ya kufanya uteuzi huo. Uteuzi huu utaanza tarehe 01/07/2016.
Dkt. Makoye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma. Dkt. Makoye mwenye Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ghana na Shahada ya Umahiri – Sanaa (M. A in Theatre Arts) toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Makoye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Idara ya Sanaa na Maonesho.
Imetolewa na,
Genofeva Matemu,
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
28 Juni,2016 (P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger