Wanajeshi wa Sudani Kusini katika uwanja wa ndege wa Bor, Kilomita 200 kaskazini mwa Juba.
Serikali
ya Sudan Kusini imetangaza kuwa watu wasiopungua 40 wameuawa katika
mapigano ya yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Wau na kubaini kuwa
huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Tume ya
umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, imeweka nyenzo maalumu za
usalama kuzunguka kambi yake iliyoko kwenye mji wa Wau, kufuatia kuzuka
kwa mapigano kati ya wapiganaji wenye silaha na wanajeshi wa Serikali,
SPLA.
Kwenye
taarifa iliyotolewa na UNMISS, imesema kuwa inaendelea kutoa ulinzi kwa
zaidi ya raia elfu 1, ambao wamenaswa kwenye mapigano yaliyoanza
mwishoni mwa juma lilillopita.
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa baada ya kufikiria kwa kina, iliamua kufungua
milango yake siku ya Jumapili na kuruhusu mamia ya raia kuingia kwenye
kambi yake, wakikimbia mapigano hayo.
Waziri wa Habari Michael Makuei, amesema kuwa maiti za raia 39 zimepatikana ikiwa ni pamoja na maiti nne za askari polisi.
Katika
taarifa iliyotolewa na wakuu wa jimbo la Wau, baada ya kikao cha baraza
la usalama la mji huo toka kulipozuka mapigano hayo Jumamosi ya wiki
iliyopita, mkuu wa polisi kwenye mji huo, Chol Thuc amesema hali imeanza
kurejea kama kawaida.
Msemaji
wa jeshi la Sudan Kuisni alisema kuwa vikosi vyake vilipigana na makundi
yaliyokuwa yamejihami pamoja na wale waliowataja kuwa wapiganaji wa
makabila.
Mashirika
ya kutetea haki za binadamu yameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa
mapigano kwenye mji huo, ambapo maelfu ya raia wameendelea kuyakimbia
makazi yao kwa hofu ya kiusalama.
Mashirika
hayo yanautaka umoja wa Mataifa kuingilia kati hali hiyo, kwa
kuvisaidia vikosi vya Serikali kukabiliana na makundi ya wapiganaji
wenye silaha ambao wameendelea kutekeleza mashambulizi ya kushtukiza
kwenye maeneo mengi ya nchi.RFI
SHARE








No comments:
Post a Comment