Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga
(Mb.) akihutubia katika Hafla ya kuadhimisha miaka mitatu ya uongozi wa
Baba Mtakatifu Papa Francis na Kumuaga Balozi wa Vatcan hapa nchini
aliye maliza muda wake wa uwakilishi.
Hafla ambayo ilifanyika jana katika viwanja vya kanisa la Mt. Petro Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Baba Mtakatifu na Vatican hapa nchini Balozi Francisco Montecillo
Padilla, akihutubia katika Hafla hiyo ambapo alitumia fursa hiyo
kuipongeza Serikali ya Tanzania na watu wake kwa ukarimu, upendo pia
ushirikiano aliokuwa akiupata kwa kipindi chote alichokuwa anawakilisha
Taifa lake hapa nchini.
Kutoka
kulia ni Kardinal Pengo, Mke wa Rais wa awamu ya tatu, Mama Anna Mkapa
na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Askofu Tarcisio
Ngalalekumtwa wakifurahia jambo kwa pamoja.
Sehemu ya Mabalozi waliohudhuria Hafla hiyo.
Waziri Mahiga akisalimiana na Kadinali Pengo wakati wa ghafla hiyo
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini W. Mkapa akizungumza na Dkt. Mahiga.
Mkuu
wa Mabalozi hapa nchini Mhe. Ambrosio Montecillo Balozi wa Angola
akizungumza na mmoja wa Maaskofu waliokuwepo kwenye Hafla Hilo
Mkurugenzi
wa Idara ya Amerika na Ulaya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza kushoto),
akizungumza na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe. Egon Kochanke
Askofu Francisco Montecillo Padilla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kuadhimisha miaka mitatu
ya Uongozi wa Baba Mtakatifu Papa Francis pamoja na kumuaga Balozi wa
Vatican na muwakilishi wa Papa hapa nchini Askofu Francisco Montecillo
Padilla ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini.
Hafla hiyo ilifanyika jana jioni katika viwanja vya Parokia ya Mtakatifu Petro Osterbay Jijini Dar es Salaam.
Katika
hafla hiyo Mhe. Mahiga alimpongeza Papa Francis pamoja na kumuelezea
kuwa ni mtu wa Mataifa yote na mfano wa kiongozi bora duniani kwakuwa
misingi yake ya uongozi imejikita katika kusimamia utu, kupinga Ubaguzi
wa rangi pamoja na matabaka katika jamii. Pia amekuwa mpiganaji mkubwa
katika masuala ya amani na mtetezi wa wakimbizi hivyo Tanzania na Dunia
nzima inatambua mchango wake kwa ujumla na kuzidi kumwombea mafanikio
katika utendaji wake.
Vilevile
alimpongeza Askofu Francisco Montecillo Padilla ambaye amekuwa
akihudumu nchini kwa muda wa miaka minne (4) na kueleza kuwa amekuwa
mfano bora katika kazi za kichungaji kwa kuweza kutembelea nchi nzima
katika Majimbo ya Kanisa Katoliki licha ya kazi yake kuwa na changamoto
nyingi. Alikumbusha tukio la mlipuko lililotokea kanisani mjini Arusha
wakati Askofu Padilla akiendesha Ibada, ni mfano dhahiri wa kazi
alizokuwa akizifanya nchini na katika hilo amejiwekea historia katika
huduma yake ya kichungaji.
Kwa
upande wa ushirikiano baina ya Tanzania na Vatican, Mhe. Mahiga alieleza
ni wa muda mrefu tangu 1960. Katika kuhakikisha uhusiano huo unaimalika
mataifa hayo mawili yamekuwa yamekuwa yakifanya jitihada za makusudi
katika kukuza uhusiano huo na alieleza hilo lilidhihirishwa na ujio wa
Papa John Paul wa pili ambaye alifanya ziara nchini Tanzania mwaka 1990.
Pia
alieleza Mhe. Rais Magufuli anapenda kutoa shukurani za dhati kwa huduma
ambazo zimekuwa zikifanywa na Balozi wa Papa nchini pamoja na Kanisa
Katoliki katika kuchangia shughuli za maendeleo hasa katika sekta ya
Afya na Elimu ambapo wamefungua Shule za ufundi za Don Bosco katika
Mikoa yote ."Ni imani yangu kuanzishwa kwa shule hizo hakutaishia katika
ngazi ya mikoa tu, bali utaendelea katika ngazi ya wilaya na hata kata"
Aidha,
alizungumzia sera ya viwanda ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli katika
kuondoa tatizo la kukosa ajira na kukuza uchumi wa Taifa, alimweleza
Balozi huyo ni muda muafaka sasa mataifa hayo mawili yakajikita zaidi
katika kuhakikisha yanaibua maeneo mapya ya ushirikiano ili kuhakikisha
sera hiyo inafikiwa kwa kuvutia zaidi wawekezaji na kukuza biashara.
Watu
wengine mashuhuri waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais mstaafu wa
awamu ya tatu Mhe. Benjamin W. Mkapa na mke wake Mama Anna Mkapa,
Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wawakilishi wa Mashirika
ya Kimataifa, Kadinali Polycarp Pengo na Maaskofu wa Majimbo ya Kanisa
Katoliki nchini, wengine ni Watawa na Walei.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dar es Salaam, 21 Juni 2016.
SHARE








No comments:
Post a Comment