Mhasibu
kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw.Willium Brown Nyamtiga
akisisitiza jambo kwa viongozi wa Chama cha Alliance for Democratic
Change (ADC) Jana wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za
chama hicho zilizopo Jijini Buguruni Dar es salaam .
Zoezi la
uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili wa Vyama va Siasa kwa
upande wa Tanzania Bara linaendelea .Tayari vyama 18
vimekwishakuhakikiwa. Vyama vinne vinatarajiwa kuhakikiwa Julai 4.
Zoezi hili ni zoezi la kawaida na endelevu ambalo hufanyika kila mwaka
ili kupima endapo vyama vya siasa vinakidhi matakwa ya Sheria ya
usajili wa vyama vya Siasa.
Uhakiki
wa Vyama vya siasa ni zoezi muhimu sana kwa sababu ni zoezi ambalo
hugusa uhai wa kila chama cha siasa. Kwa upande wa Tanzania Visiwani ,
uhakiki unatarajiwa kuanza mara baada ya kumalizika Bara kwa tarehe
ambazo zitatangazwa baadaye.
Bw.Eugene
Kabendera, Katibu Mwenezi Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
akitoa taarifa wa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya
Siasa wakati wa Zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi za chama hicho
zilizopo Jijini Makumbusho Dar es salaam Juzi
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama cha Jahazi Asilia, Bw. Mbwana S. Kibanda akifafanua
jambo wakati wa zoezi la uhakiki liliofanyika Leo katika ofisi za
chama hicho zilizopo ilala Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa
chama hicho na kushoto ni watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa. (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment