Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema) wilaya ya Temeke
kimemfukuza uanachama Diwani wa Kata ya Kurasini ambaye ni mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Mivinjeni , Matiti Togocho
kwa kile walichodai
kuwa amekuwa akifanya ufisadi ikiwemo kutengeneza hati za viwanja feki
na kujipatia kipato.
Mwenyekiti Chadema wilaya hiyo Berdad Mwakyembe
amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na makosa ya ufisadi
aliyowafanyia wananchi wa kata yake.
Mwakyembe alisema diwani huyo
ameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake badala yake alikuwa
anatumia nafasi yake kujinufaisha huku akiwawakandamiza wananchi
wanyonge.
Hata hivyo Diwani Togocho alisema hatozungumzia suala hiko hadi atakapopewa ruhusa kutoka kwa mratibu wa kanda kuongea suala hilo
Hata hivyo Diwani Togocho alisema hatozungumzia suala hiko hadi atakapopewa ruhusa kutoka kwa mratibu wa kanda kuongea suala hilo
“Unajua
aliyeongea mwenyekiti wangu hivyo siwezi kuropoka kitu hadi nisikilize
mabosi wangu ambaye mratibu wa kanda,”alisema Togocho.
Source:- Mwananchi/Citizen
SHARE
No comments:
Post a Comment