Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiangalia athari ya tetemeko katika eneo
la Shule ya Msingi Bieju Kata ya Mtukula wakati alipowasili Wilayani
Misenyi kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo yaliyoathirika
na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea maelezo juu ya idadi na thamani ya
uharibifu katika shule ya Sekondari Mtukula toka kwa Mkuu wa Wilaya ya
Misenyi, Luteni Kanali Denice Filangali Mwila wakati alipowasili
Wilayani hapo kwa ajili ya ziara ya kushuhudia baadhi ya maeneo
yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21 Septemba, 2016.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiongea na wakazi wa Kata ya Bugandika,
Wilayani Misenyi wakati alipofanya ziara Wilayani hapo kushuhudia baadhi
ya maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera leo 21
Septemba, 2016. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.
Na Benedict Liwenga-WHUSM, Kagera.
SERIKALI imetibu wananchi bure ikiwa ni sehemu ya msaada wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Kauli
hiyo imetolewa leo Mkoani Kagera na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama
wakati alipofanya ziara Wilayani Misenyi kushuhudia baadhi ya maeneo
yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi.
Mhe.
Mhagama ameeleza kuwa, Serikali hadi hivi sasa imewatibu watu zaidi ya
400 kupitia hospitali zake za Wilaya na Mkoa kwa kuagiza madaktari
kutoka nchini China ambapo zoezi la kusambaza damu pamoja na dawa za
kutosha kwa waathirika lilifanyika na hakuna mwananchi aliyetozwa fedha
kama malipo ya huduma hiyo.
“Tuishukuru
Serikali yetu kwa kutusadia kupata dawa na damu ya kutosha na
tulihakikisha kuwa kila mtu aliyepatwa na tetemeko na kujeruhiwa
anatibiwa kwa gharama za Serikali ndiyo maana tuliagiza madaktari kutoka
China pamoja na Mwanza ili kusaidia kuwatibu wananchi waliopatwa na
majeraha makubwa”, alisema Mhe. Mhagama.
Aliongeza
kuwa jumla ya wagonjwa ambao kwa sasa wanaendelea kutubiwa hospitalini
ni 23 na ndiyo ambao wamefanyiwa upasuaji mkubwa na hali zao zinaendelea
vizuri tofauti ilivyokuwa hapo awali.
Alifafanua
kuwa, Serikali haiwezi kumsaidia kila mtu kwani haina uwezo huo lakini
inajitahidi kurejesha miundombinu yake na taasisi zake zikiwemo
zahanati, shule barabara kwa kushirikiana na wadau wanaojitokeza kuunga
mkono juhudi za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo, hivyo ametaka
wananchi kujitokeza na kushirikiana kwa pamoja katika kuwasaidia
waliopatwa na tukio hilo.
Naye Mkuu
wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa
katiika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo
jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa
mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71
za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko
hilo.
Ameongeza
kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati
ya Maafa ni ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo
mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika
pia.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka
wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa ambapo
amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.
Hivi
karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na
ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli
ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi
kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri. (P.T)
Moja ya malori yaliyoteketezwa
Marekani
na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria,
pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano.
Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo.
Waziri wa
Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi John Kerry, alitoka nje ya lugha ya
kidiplomasia kwa kutumia dhihaka zaidi. Huku mwenzake wa Urusi Sergey
Lavrov akipinga hisia hizo kali kwa kuorodhesha mifano kadhaa kutetea
nchi yake. Aidha ametaka pia kufanyika
Licha ya
majibizano makali, Urusi na Marekani zilikubaliana kwa pamoja kuongoza
mkutano wa mataifa 23, yanayoiunga mkono Syria ambao utafanyika mjini
New York, baadaye leo.
Katika
hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unajiandaa kuanza tena kutoa
misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria, baada
ya kusitishwa kwa usambazaji wa misaada kufuatia shambulio hilo.
Mjumbe wa
Umoja wa Mnataifa nchini Syria, Staffan de Mistura ameiambia BBC kwamba
misafara hiyo ya misaada itaanza katika baadhi ya maeneo lakini kwa
uangalifu na tahadhari kubwa. Misaada hiyo amesema haitasambazwa katika
eneo linaloshikiliwa na waasi la Aleppo, ambalo limeshambuliwa vibaya. BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment