Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini(Taswa FC),Wilbert
Molandi katika fainali la Bonanza la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha
kwenye uwanja wa General Tyre jumapili,kulia ni Mwenyekiti wa Taswa
FC,Majuto Omary na kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo,Mussa Juma.
Nahodha wa timu ya Netiboli ya
Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers
Association Sports Club (Taswa SC)Zuhura Abdulnoor na mchezaji mkongwe
wa Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini,(Taswa FC),Muhidin Sufiani(kulia)wakifurahia ushindi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha.
Mchezaji nguli wa timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini(Taswa FC),Muhidin
Sufiani akichanja mbuga kupenya ngome ya timu ya Chuo cha Uandishi wa
Habari Arusha(AJTC)katika mchezo wa fainali ambao Taswa FC walishinda
bao 1-0.
Wachezaji
wa Netiboli wa Taswa SC na Chuo cha Uandishi wa Habari
Arusha(AJTC)wakichuana vikali katika bonanza hilo ambalo Taswa
SCMwalibamiza bila huruma 30-2
Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezonchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na waratibu wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.
Na Mwandishi wetu-Arusha.
Timu ya soka ya waandishi wa Habari za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo
nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) zimetwaa ubingwa wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.
nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) zimetwaa ubingwa wa bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.
Taswa FC
na Taswa Queens ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini
ya Acacia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) zilifanikiwa kushika nafasi
ya kwanza katika bonanza hilo la kusisimua na waandishi kushindana
katika michezo mbalimbali mbali ya soka na netiboli.
Timu ya
Wazee Club ambao ilishika nafasi ya pili, ndiyo pekee iliyonusurika na
kichapo katika bonanza hilo aada ya kuambulia sare ya mabao 2-2. Hata
hivyo, timu hiyo ilibidi ifanya kazi ya ziada baada ya kusawazisha mabao
mawili katika dakika sita za mwisho.
Timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji cha AJTC kilishika nafasi ya tatu na timu ya mwisho ni Redio Sunrise.
Taswa FC
ilianza kwa kasi na kufunga mabao mawili ya haraka haraka kupitia kwa
Saidi Seifu akipokea pasi safi za Majuto “Dr Regret” Omary. Martin
Shila, Edrward Mbaga, Muhidin Sufiani, Zahoro Mlanzi, Salum Jaba na kipa
wao, Mwarami Seifu walikuwa kizingiti kikubwa katika mechi zote.
Katika
mechi ya pili, Taswa FC ilishinda mabao 4-0n dhidi ya Sunriseb Redio ,
bao la kwanza likifungwa na kapteni, Wilbert Molandi kwa kuunganisha
kona ya Hare Temba na baadaye Saidi Seifu akifunga mabao matatu kufutia
pasi ya Athumani Jabir na Majuto Omary ambaye alitoa pasi ya bao la tatu
na la nne.
Katika
mchezo wa mwisho, Taswa FC iliibuka na ushindi wa ba 1-0 dhidi ya AJTC,
bao la dakika za majeruhi lilifungwa na Ali “Maradona” Salum kufuatia
kona safi ya Majuto.
Timu ya
netiboli ya Taswa Queens ilifanya ‘mauaji’ kufuatia ushindi wa mabao
30-2 dhidi ya AJTC. Mabao ya Taswa Queens yalifungwa na Sharifa Mustapha
aliyefunga mabao 22 na Rose Michael aliyefunga mabao nane.
Taswa
Queens ilitawala sana mchezo huo kupitiaa wachezajia wake, Zuhura
Abdinoor, Johari William, Elizabeth Mbasa, Tatu, Mage na Vicky Godfrey.
Timu zote
hizo zilizawadiwa kitita cha sh 100,000 kila moja na kombe. Kwa upande
wa kukimbiza Kuku, Taswa Queens pia walifanikiwa kuibuka na ushindi
wakifuatiwa na Sunrise Radio ambao wote waliondoka na kuku kila mmoja.
Mgeni
rasmi katika bonanza hilo la 11 lillilofanyika katika viwanja vya
General Tyre alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro
ambaye alisema kuwa waandishi wa habari ni muhimu kushiriki michezo ya
aina mbalimbali ili kuiweka miili vizuri. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment