Mkuu
wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda akishirikiana na
wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Temeke kukata utepe kuashiria uzinduzi
wa Tawi la Temeke jijini Dar es Salaam.
BENKI
ya Exim imefanya maboresho ya huduma zinazotolewa kwa wateja wake wa
maeneo ya Temeke, jijini Dar es Salaam kwa kufungua tawi jipya ambalo
lina maboresho mengi tofauti na jengo ambalo walikuwa wakilitumia awali.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim,
Seleman Mponda amesema kwasasa wamedhamiria kuboresha huduma zao katika
maeneo mbalimbali na kuahidi wateja kuendelea kuwapatia huduma bora.
“Benki
yetu inaendelea kufanya vizuri na tumejipanga kuendelea kuboresha
huduma zetu, mwanzoni tulikuwa sehemu nyingine na wateja wetu walikuwa
wakituuliza lini tutahamia sehemu iliyo na nafasi nzuri ya kutoa huduma
na sasa tumeipata,” alisema Mponda.
Meneja
wa Tawi la Benki Exim Temeke, Subira Augustino akiwakaribisha wageni
waalikwa ndani mara baada ya ufunguzi kufanyika wa Tawi la Exim Bank
Temeke.
Meneja
wa Tawi la Benki Exim Temeke, Subira Augustino akitoa neno la
ukaribisho kwa wafanyakazi wa Exim Benki na wateja ambao walialikwa kwa
ajili ya kushuhudia hafla ya ufunguzi wa Tawi la Exim Temeke.
Mkuu
wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda akizungumza
kuhusu benki ya Exim na jinsi ambavyo wamejipanga kuboresha huduma.
Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Wadogo Wadogo wa Banki ya Exim, Raul Singh
akielezea jinsi Exim Bank ambavyo inazidi kufungua matawi maeneo mengine
ili kuwasogezea wateja huduma kwa ukaribu.
Wageni
waalikwa wakikata keki. Wa kwanza kushoto (mwenye suti nyeusi) ni Mkuu
wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda, Mteja wa Benki ya
Exim, Abdelsamad Hussein, Afisa Mauzo wa Benki ya Exim Temeke, Rashid
Bundara, Mteja wa Benki ya Exim, Saamu Omary, Mteja wa Benki ya Exim,
Shukran Ezekiel.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda akimlisha keki Mteja wa Benki ya Exim, Abdelsamad Hussein.
Meneja wa Tawi la Benki Exim Temeke, Subira Augustino akimlisha keki Mteja wa Benki ya Exim, Saamu Omary.
Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Wadogo Wadogo wa Banki ya Exim, Raul Singh
akiwagawia keki baadhi ya wateja wa benki hiyo ambao walijumuika nao
pamoja katika uzinduzi wa Tawi la Exim Bank Temeke.
Baadhi ya wateja wa Exim Bank wakitoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wa benki hiyo.
Wafanyakazi wa Exim Bank wakiwa katika picha ya pamoja.
Wafanyakazi
wa Exim Bank wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wao waliohudhuria
halfa ya ufunguzi wa Tawi la Exim Bank Temeke.
No comments:
Post a Comment