| Habari Picha na Woinde Shizza,Arusha Ajali za pikipiki kwa mkoa wa Arusha zimeongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 zilifika ajali 836 huku upande ajali za magari zikipungua kwa asilimia 11. |
Hata
hivyo ajali hizo za pikipiki kwa mwaka 2010 zilikuwa 709 ukilinganisha
na ajali 277 za pikipiki mwaka 2009 ajali hizo za pikipiki bado
zinaendelea kuongezeka.
Hayo
yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani
wakati akielezea hali ya usalama wa barabarani kwenye uzinduzi wa
maazimisho ya wiki ya usalama barabarani mapema leo.
Selemani
alisema kuwa takwimu zinaonesha mkoa wa Arusha bado unakabiliwa na
ajali za barabarani ambapo kwa kipindi cha mwaka 2007 ajali zimekuwa
zikiongezeka na kulikuwa na ajali 1807na kufikiakiwango cha juu mwaka
2010 ambapo ajali 2658 huku kwa kipindi cha mwaka 2012 ajali zilianza
kupungua hadi kufikia ajali 2011
Alifafanua
kuwa baada ya jeshi kutumia nguvu kubwa sana katika kupunguza ajali
zinazotokana na magari zilipungua sana ingawaje kwa sasa bado wimbi
kubwa la ajali linatokana na ajali za pikipiki.
Katika
hatua nyingine alisema kuwa ajali zinasababishwa na sababu za
kibinadamu kwa asilimia 75,madereva kulewa huku wakiwa wanaendesha
vyombo vya moto,pia ubovu wa vyombo vya usafiri kwa asilimia
15,miundombinu ya barabara kwa asilimia10.
Awali
mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro
alisema jukumu la usalama wa barabarani sio la polisi wenyewe wala
kamati ya kikosi cha usalama barabarani pekee bali ni ulinzi wa kila
mtu.
Fabian
alisema kuwa endapo kama kila mtu atafuata sheria na kanuni za
barabarani basi ajali zitakuwepo kwa kiwango cha asilimia 0.0 kwani
ajali zinachangia kudidimiza mlengo wa taifa.
Hataivyo
katika uzinduzi huo baadhi ya askari wa usalama barabarani walifanikiwa
kupewa vyeti vya ufanyakazi bora ambapo mmoja wa askari hao Silas Konga
alisema kuwa maadili yao bora kazini yamechangia wao kutambulika na
jeshi hilo.
Askari wa
usalama barabarani koplo Atilio Choga akiwa anatoa maelezo mafupi ya
barabara zilizopo mkoani Arusha na jinsi magari yanavyoingia na
kutoka katika siku ya uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani
ilianza Jana katika viwanja vya sheikh Amri Abeid ,mbele ni mkuu wa
wawilaya ya Arusha Fabian Daqarro ambapo alikuwa mgeni
rasmi
askari polisi wa kikosi cha
usalama barabarani akimuonyesha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya
ya Arusha jinsi kifaa chakupimia ulevi kwa madereva kinavyo fanya
kazi
kabla ya sherehe kuanza
kulikuwa na maaandamano apa askari wa kikosi cha usalama
barabarani wakiwasili katika viwanja vya sheikh Amri Abeid kwa
maandamano
kikundi cha walemavu wao pia
walijitokeza katika sherehe hizi za uzinduzi wa siku ya usalama
barabarani
kikundi cha ngoma cha wanafunzi nacho
kilikuwepo katika sherehe hizi za siku ya usalama
barabarani
wageni waalikwa wakiwa
wanafatilia uzinduzi huo leo katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh
Amri Abeid
kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani
akiwa anasoma risala
| mkuu wa wilaya ya
Arusha Fabian Daqaro katikati akiwa anaandika baadhi ya changamoto
alizotajiwa |
SHARE








No comments:
Post a Comment