Mhe
Joseph Mkirikiti akikabidhi lebo za vifungashio kwa Bi Safina Selemani
mzalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka kata ya Nandagala B kikundi cha
CHIUKUTE, lebo hizo zimetengenezwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
ya Tanzania (TanTrade)
Mkuu
wa Wilaya ya Ruangwa Mhe Joseph Mkirikiti akipokea lebo za vifungashio
kwa wazalishaji wa mafuta ya alizeti katika mkoa wa Ruangwa kata ya
Nandagala B kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara ya Tanzania (TanTrade) Bw Edwin Rutageruka
MAFUNZO
YA UFUNGASHAJI BORA, KUWEKA NEMBO, RAJAMU NA MASOKO (MASASI &
RUANGWA) NA KUTOA LEBO KWA WAZALISHAJI WA MAFUTA YA ALIZETI
Mhe
Joseph Mkirikiti Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ahimiza uzalishaji wa mafuta
ya Alizeti, Ufuta na Nazi kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa sababu ni
kioo na msingi imara ya kuwawezesha ajira iwe ya kudumu na tena ajira
bora kwa wananchi.
Hayo
aliyasema akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa vitendo kwa
wakulima ambao ni wazalishaji wa bidhaa za mbegu za mafuta ya ufuta,
nazi na alizeti wa Ruangwa na akipokea lebo za vifungashio vya mafuta ya
alizeti kwa wazalishaji wa bidhaa za mafuta ya alizeti zaidi ya 1000
zilizotengezwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Mafunzo
hayo yameanza tarehe 7 hadi 10 Novemba, 2016 juu ya namna ya
ufungashaji bora wa bidhaa za mbegu za mafuta ya ufuta, alizeti na nazi,
kuwa na lebo bora kwenye kila bidhaa inayozalishwa, rajamu (branding)
kwenye bidhaa hizo, namna ya kuboresha ubora wa bidhaa na mbinu ya kuuza
bidhaa hizo kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi kwa wazalishaji
wapatao 50 wa Ruangwa na 50 wa Masasi.
“Elimu
mtakayopata hapa itawachukueni kwenye hatua nyingine ya kufanya
maboresho makubwa ya ajira yenu, hapa nchini mahitaji ya mafuta ya kula
kwa mwaka ni lita 350,000 wakati uzalishaji kwa sasa ni asilimia 40
pekee na asilimia 60 huagizwa kutoka nje ya nchi hivyo basi, tuna fursa
kubwa ya kunufaika na sekta hii.”
Akasisitiza
kuwa ni vyema kusikiliza na kutumiamafunzo hayo kwa makini na kwenda
kuambukiza elimu hiyo kwa wengine waliokosa kuhudhuria mafunzo haya ili
kwa pamoja kama Taifa tufanye biashara yenye faida na kufikia malengo ya
Taifa na mtu mmojammoja.
Mhe
Mkirikiti aliendelea kusema kuwa Ruangwa iwe mstari wa mbele sasa katika
kuzalisha bidhaa zenye ubora na kupitia msaada wa lebo kutoka TanTrade
na vifungashio bora ili bidhaa zionekane kwenye macho ya mlaji kabla ya
kutumia na kuleta ufahari kwa nchi ya Tanzania pindi bidhaa zetu
zitakavyoweza kuvuka nje ya nchi hivyo watumie mafunzo hayo kutangaza
bidhaa zetu bora zaidi.
Alieleza
kuwa anaimani kupitia mafunzo haya yataboresha pia maeneo ya kazi ili
ubora usipungue na pia wakiendelezwa wajasiliamali wadogo kutapelekea
kuanzishwa viwanda vidogo vingi zaidi na kuongeza tija kwenye uzalishaji
wa mafuta na maendeleo kuja kwa haraka sana na kupunguza kwa kiwango
kikubwa kuagiza mafuta kutoka nje.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendelo ya Tanzania (TanTrade) alisema
moja ya kazi ya taasisi ni kuwajengea uwezo na kuwaendeleza wazalishaji
wadogo, hivyo imeandaa mafunzo haya kwa ushirikiano wa wadau wa
kimkakati ambao ni SIDO na TBS ilikuimarisha fursa kwa wakulima
kuzalisha kitu cha thamani ili kuweza kuleta ushindani katika soko la
ndani na nje ya nchi.
“Mwezi
Agosti kwenye maadhimisho ya siku ya wakulima (88), TanTrade ilifanya
ziara fupi kwenye wilaya za Ruangwa, Masasi na Kilwa na pia kupita
kwenye mabanda ya washiriki kubaini fursa zilizopo kwenye mikoa ya Lindi
na Mtwara kupitia vikundi mbalimbali vilivyoshiriki maadhimisho hayo
ili kuendeleza fursa hizo kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya
nchi.”
Akaongeza
kwa kusema kuwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade)
ilipobaini changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye kilimo biashara
(Agribusiness) hivyo ikaona ni vyema kutatua changamoto hizo kwa kuanza
kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa hizo kwa kutoa mafunzo kwa
vitendoyatakayojikita kwenye mbinu za kutafuta masoko na mikakati ya
kuingia sokoni, uzalishaji wa viwango vyenye ubora wa mbegu za mafuta
(Alizeti, Ufuta na Nazi) na vifungashio vya mafuta hayo, Nembo ya
utambulisho wa bidhaa zao (lebo) na elimu juu ya mfumo wa matumizi ya
simbomilia (barcode) na nembo ya ubora katika wilaya ya Ruangwa na
Masasi na kuwatengeneza lebo ili bidhaa zao ziweze kutambulika kwenye
masoko yao.
Akishukuru
kwa niaba ya kikundi cha CHIUKUTU kilichopo kata ya Nandagala B wilaya
ya Ruangwa Bibi Safina Selemani baada ya kupokea lebo kwaajili ya bidhaa
zao kutoka kwa Mkuu wa Wilaya alisema changamoto kubwa ilikuwa ni
ukosefu wa elimu ya namna ya uboreshaji wa uzalishaji bora wa bidhaa za
mafuta, hivyo ni fursa ya pekee kwao kupatiwa mafunzo na lebo hizo ili
kujiendeleza kwenye uzalishaji.
SHARE










No comments:
Post a Comment