Shirika la kimataifa la haki za binaadamu, Amnesty International,
limesema mwaka 2016 ulikuwa mwaka mbaya kwa haki za binaadamu, huku
uhalifu wa kivita ukiwa umefanywa duniani kote. Hayo yamo katika ripoti
mpya ya shirika hilo iliyotolewa leo ambayo inaeleza jinsi wakimbizi
walivyoandamwa, huku mataifa yenye nguvu duniani yakishindwa kukabiliana
na changamoto hiyo. Katibu Mkuu wa Amnesty International, Salil Shetty
amesema mwaka 2016 ulikuwa mbaya kuwahi kushuhudiwa katika suala la haki
za binaadamu. Ripoti hiyo ya mwaka imehusisha utafiti kuhusu ukiukwaji
mkubwa wa haki za binaadamu kwenye nchi 159, ambapo 23 kati ya hizo pia
zilihusika na uhalifu wa kivita, ikiwemo Sudan Kusini, Myanmar na
Ufilipino. Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa moja ya tatizo kubwa la
mwaka 2016, lilikuwa ni kuongezeka kwa matamshi ya chuki kwenye maeneo
mengi ya Ulaya na Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment