Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev amemteua mkewe kuwa 'Makamu wa
Kwanza wa Rais.' Aliyev alitangaza jana kuwa mkewe Mehriban, atashika
nafasi hiyo ya pili kubwa katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.
Nafasi ya 'Makamu wa Kwanza wa Rais' ilianzishwa mwaka uliopita baada ya
kufanyika kura ya maoni, ingawa sheria haijaeleza wazi majukumu halisi
ya kiongozi huyo. Wabunge wa upinzani wameukosoa vikali uteuzi huo,
wakisema hayo ni matumizi mabaya ya madaraka na ndiyo mwanzo wa
kuanzishwa utawala wa kifalme. Aliyev tayari amekosolewa na mashirika ya
haki za binaadamu kutokana na hatua yake ya kukandamiza uhuru wa
kujieleza, kuzuia uchaguzi huru na wa haki pamoja na kuwafunga wapinzani
wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment